Ni
taarifa ya kushtusha sana ya msiba wa mwanasiasa chipukizi na jasiri,
Deo Filikonjombe kutokana na ajali ya Helikopta jana jioni(juzi) maeneo
ya mbunga ya Selous mkoani Morogoro.
Ni
pigo lingine kubwa ambalo katika kipindi kifupi Taifa limepata, huku
bado likiwa na kidonda cha kuondokewa na wana siasa wengine
mahiri,Marehemu Celina Kombani, Dr Abdallah Kigoda na Dr Emanuel Makaidi
aliyefariki jana(juzi)
Filikonjombe
alikuwa Mbunge mahiri aliyesimama imara kutetea maslahi ya wananchi wa
jimbo lake la Ludewa na watanzania kwa ujumla.
Alikuwa
mwiba kwa serikali ya Chama chake CCM kutetea maslahi ya nchi, mfano ni
katika kashfa ya Escrow ambapo alikuwa Makamu Mwenyekiti wa kamati
iliyochunguza kashfa hiyo.
Mwenyezi
mungu awape moyo wa subira, familia, jamaa, marafiki na wananchi wa
Ludewa, katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.
BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.-Edward Ngoyai Lowassa
No comments:
Post a Comment