MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo itatoa uamuzi kuhusu shauri la kikatiba lililofunguliwa na Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Amy Kibatala likihoji uhalali wa wapigakura kukaa mita 200 kutoka kwenye vituo vya kupigia kura.
Mwenyekiti
wa Jopo la Majaji watatu linalosikiliza kesi hiyo, Sekieti Kihiyo
alisema Dar es Salaam jana wakati akiahirisha kesi hiyo iliyotajwa kwa
ajili ya maelekezo muhimu alisema, uamuzi huo utatolewa saa 4:00
asubuhi. Pamoja na Jaji Kihiyo, majaji wengine wa kesi hiyo ni Lugano
Mwandamba na Aloycius Mujulizi.
Kesi
hiyo ilitajwa jana kwa ajili ya maelekezo muhimu. Kesi hiyo
imefunguliwa na Amy anayegombea ubunge Viti Maalumu Jimbo la Kilombero,
Morogoro, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), pamoja na
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC).
Amy
anaiomba Mahakama itoe tafsiri ya Kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya
Uchaguzi Sura ya 343 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010, kinachohusu
uhalali wa wananchi kukaa meta 200 kutoka katika kituo cha kupiga kura.
Kesi
hiyo ilianza kusikilizwa juzi ambapo Naibu Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Dk Tulia Ackson akisaidiwa na jopo la mawakili wanane,
aliiomba Mahakama itupilie mbali kesi hiyo kwa kuwa kifungu cha sheria
kilichotumika siyo sahihi na pia mlalamikaji hajaeleza jinsi gani haki
yake itakiukwa.
No comments:
Post a Comment