HATIMAYE MGOMBEA URAIS TLP APIGA KURA YAKE - LEKULE

Breaking

25 Oct 2015

HATIMAYE MGOMBEA URAIS TLP APIGA KURA YAKE


Mgombea urais kwa tiketi ya Tanzania Labour Party (TLP), Maximillian Lyimo.
Mgombea urais kwa tiketi ya Tanzania Labour Party (TLP), Maximillian Lyimo hatimaye amepiga kura yake katika Kituo cha Njia Panda, Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Awali Mhe. Lyimo alishindwa kupiga kura baada ya kukosekana taarifa zake kituoni hapo.
Lyimo aliyejiandikishia mkoani Dar es Salaam, jana alienda kufunga kampeni zake Jimbo la Vunjo na kulala huko, asubuhi ya leo alienda kituo cha Njia Panda jimboni humo ili akapige kura.
Baada ya kufika kituoni hapo akiwa na kitambulisho chake cha kupigia kura, alizuiwa baada ya kukosekana fomu namba 19 ambayo kisheria inamuwezesha mgombea urais kupiga kura ya kumchagua rais kwenye kituo chochote.
Mbali na Lyimo kupiga kura, mlinzi wake aitwaye Wile ambaye ni inspekta wa polisi yeye kazuiliwa kabisa kupiga kura yake.

No comments: