Haji Duni agundua janja ya CCM,waliopangwa kuchakachua matokeo watajwa - LEKULE

Breaking

24 Oct 2015

Haji Duni agundua janja ya CCM,waliopangwa kuchakachua matokeo watajwa

Mgombea Mwenza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Haji Duni amesema kuwa wamegundua njama iliyopangwa na Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Tume ya uchaguzi kwamba kura zikitoka kwenye vituo zipite kwenye mtandao na kuziiba kwa kutumia wataalamu wao wa TEHAMA.
 
Ameyasema hayo mapema leo wakati wa kufunga kampeni kwa vyama vinavyounda umoja huo zilizofanyika katika viwanja vya jangwani jijini Dar es Salaam
 
Duni  amesema kuwa CCM imetayarisha wataalam wawili ambao watafanya kazi hiyo na kwamba UKAWA watajitahidi kuweka kumbukumbu iliyosahihi ya matokeo ya kura zao zote ili kuepusha wizi unaotaka kufanywa.
 
Ameongeza kuwa kila wakala lazima apatiwe nyaraka ya matokeo ya kura iliyotiwa saini,
 
Aliwataja wataalam hao kuwa ni Mr Mkanyanga na Sesy Francis ambao ndio wamekabidhiwa kuiba kura katika kituo cha Kurasini karibu na makao makuu ya uhamiaji.
 

“Wakileta mchezo tutawaambia wananchi wakakizunguke alafu tutaona kama hodari ni Rais Kikwete au wananchi …..Kikwete umeambiwa ukabidhi nchi kama ulivyopewa kwa amani na akuna Jeshi linaloweza kupiagana na umma,”amesema Duni.

No comments: