Mgombea Urais wa CCM Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwanadi Mgombea Ubunge wa Kahama Ndugu Jumanne Kishimba pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Msalala Ndugu Ezekiel Maige mbele ya maelfu ya wakazi wa mji huo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni kabla ya uchaguzi mkuu 2015
ALIYEKUWA mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba baada ya kutangazwa kuwa mshindi ameanza kazi kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni 20 kwa ajili ya kusaidia wodi ya akina mama wajawazito.
Jumanne Kishimba ambaye ni tajiri wa Mwanza na mmiliki wa maduka ya "Imalaseko Supermarket", na hii siyo mara ya kwanza kwa Kishimba kugombea nafasi hiyo, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2000 alipogombea jimbo la Msalala.
Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Kahama Mjini Anderson Msumba baada ya kumtangaza Kishimba kuwa mshindi wa jimbo hilo dhidi ya mpinzani wake James Lembeli (CHADEMA/UKAWA) alianza kutatua kero za wananchi kwa kutembelea hospitali ya Wilaya Kahama na kuwasadia akina mama wajawazito.
Akiongea na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama Bruno Minja, Kishimba alisema kuwa katika kampeni zake alipata changamoto ya kero ya matatizo ya wodi ya Akinamama wajawazito kutokana na upungufu wa Vitanda pamoja na Vifaa wakati wa kujifungua.
“Niliahidi kuwa kama nitafanifanikiwa kupata ridhaa ya kuwaongoza wanakahama, nitahakikisha kuwa ninamaliza tatizo la huduma za afya katika hospitali ikiwa ni pamoja na kuondoa tatizo la kujifungulia chini katika wodi ya Wazazi’, alisema Kishimba.
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Bruno Minja akitoa matatizo ya hospitali hiyo kwa Kishimba alisema kuwa hospitali hiyo imekuwa ikipkea wagonjwa wengi kutoka Wilaya mbalimbali zinazozunguka Wilaya ya Kahama.
Minja alisema kuwa katika wodi ya akina mama wajawazito wamekuwa wakipokea jumla ya akina mama wanaojifungua kati ya 20- 25 huku wodi hiyo ikiwa na uwezo kupokea wajawazito nane hali ambayo imekuwa ikisababisha kujifungulia sakafuni.
Mshindi huyo baada ya kutembelea wodi hiyo aliongea na wananchi na kusema kuwa masuala ya kampeni yameisha na kuwa kama kuna watu tulikwazana wakati wa kuomba kura "tusameheane, muda wa majungu umeisha, hapa kazi tu."
Mpaka kufikia hivi sasa ni matokeo ya jimbo moja tuu la Kahama Mjini ambayo yametangzwa na Mkurugnezi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama yenye kata 20 huku CCM ikishinda kwa idadi ya kata 19 na CHADEMA ikipata kata moja tu.
Wilaya ya Kahama ina majimbo matatu ya Ubunge ambayo ni Jimbo la Msalala, ambalo Mgombea wake aliyeshinda ni Ezekiel Maige huku Jimbo la Ushetu akishinda Elias Kwandikwa.
No comments:
Post a Comment