kombani
Majonzi makubwa  lufuatia taarifa za msiba  jioni ya leo Septemba 24.2015, Aliyekuwa  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeshi Kombani (56),  amefariki dunia leo huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani. 
Tayari mamlaka husika ikiwemo Serikali na Bunge  kupitia  ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kubainisha kuwa, mwili wa marehemu unategemewa kuwasili  Tanzania, siku ya Jumatatu, na shughuli zote Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko Mahenge.
Kabla ya kupatwa na umauti, marehemu alikuwa  Mbunge wa jimbo la Ulanga Mashariki na pia alikuwa akigombea ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).