25 Sept 2015
Waziri Celina Kombani afariki dunia nchini India leo, mwili wake watarajiwa kuwasili nchini JUMATATU
Majonzi makubwa lufuatia taarifa za msiba jioni ya leo Septemba 24.2015, Aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeshi Kombani (56), amefariki dunia leo huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani.
Tayari mamlaka husika ikiwemo Serikali na Bunge kupitia ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kubainisha kuwa, mwili wa marehemu unategemewa kuwasili Tanzania, siku ya Jumatatu, na shughuli zote Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa marehemu huko Mahenge.
Kabla ya kupatwa na umauti, marehemu alikuwa Mbunge wa jimbo la Ulanga Mashariki na pia alikuwa akigombea ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
‹
›
Home
View web version