Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (PICHA MAKTABA) |
Na Kahema Emanuel,Mbeya
WITO
umetolewa kwa Waratibu wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi wa uchaguzi
na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi wa halmashauri mikoa
ya kanda za juu kusini kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa waledi na kwa
uadilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa ua mgombea.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro wakati
akifungua mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi
pamoja na maafisa uchaguzi halmashauri ambao ni wakurugenzi wa
halmashauri na maafisa uchaguzi katika mikoa ya Iringa na Mbeya.
Amesema
ili zoezi hilo la uchaguzi liende vizuri na lisighubikwe na vurugu
nivema wasimamizi hao wakatumia waledi wao na udilifu bila kuwa na
upendeleo wa chama chochote cha siasa au mgombea yoyote ili kuepuka hali
hiyo.
Amesema
mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo nivema wakaendelea kutumia muda wao
wa ziada kusoma na kupitia vitabu vya maelekezo waliyopatiwa kwa
kutumia kanuni na maadili ya uchaguzi ili kuimarisha uelewa zaidi kuhusu
wajibu na majukumu yao katika zoezi hili la uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.
Amesema
pamoja na majukumu mengine waliyonayo pia wametakiwa kutoa kipaumbele
katika kutekeleza zoezi hili la kitaifa kwa ufanisi zaidi na kwa muda
uliopangwa kwani uchaguzi huu utafanyika kwa siku moja tu kwa kila baada
ya miaka mitano.
Aidha
amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetekeleza jukumu lake katika
hatua ya mafunzo na maandalizi ya vifaa na rasilimali nyingine hivyo wao
kama wasimamizi wanatakiwa kutekeleza wajibu wao katika ngazi zote kwa
mujibu wa taratibu zilizopangwa na Tume.
Katika
semina hiyo wasimamizi hao watajifunza wajibu wa wasimamizi wa vituo
vya kupigia kura ,uwendeshaji wa zoezi la upigaji kura vituoni sanjali
na uendeshaji wa zoezi la kuhesabu kura,kujumlisha kura na kutanganza
matokeo ya uchaguzi.
Afisa Uchaguzi Kanda ya Nyanda za juu kusini -Tume Ndugu Jane Tungu akizungumza katika semina hiyo. |