Joseph kabila
Wanasiasa
saba waandamizi wamefurushwa kutoka kwa serikali ya muungano katika
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo baada ya kumuandikia rais wakimtaka
kutokwamilia madaraka, kulingana na maafisa.
Katika
barua kwa Joseph Kabila,viongozi wa G7,kundi lenye vyama ndani ya
muungano huo lilitaka hatua kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa uchaguzi
unafanyika kufikia mwezi Novemba.
Mda wa kikatiba wa rais Kabila unakamilika mwaka ujao,lakini amekataa kuthibitisha kwamba hatowania muhula mwengine.
Upinzani pia unahofia kwamba uchaguzi huo utacheleweshwa.
wanasiasa wa DRC
Ulifanya mkutano wa kisiasa katika mji mkuu wa Kinshasa hapo siku ya jumanne ili kumtaka rais Kabila ajiuzulu mwaka ujao.
Msemaji
wa serikali Lambert Mende alikana kwamba bwana Kabila alitaka kukiuka
katiba kulingana na n chombo cha habari cha Reuters
No comments:
Post a Comment