Rais wa
Burkina Faso Michel Kafando (kushoto) Na Luteni Kanali Isaac Zida,
katika sherehe ya kupeana madaraka, Novemba 2014, Ouagadougou.
Na RFI
Wanajeshi
kutoka kikosi cha usalam wa Rais wanamshikilia tangu Jumatano mchana
wiki hii Rais wa Burkina Faso, Waziri Mkuu Isaac Zida pamoja na mawaziri
kadhaa, baada ya kuingia ghafla katika Ikulu wakati wa kikao cha Baraza
la mawaziri mjini Ouagadougou.
Hali bado
ni tata katika Ikulu ya Kosyam , makao makuu ya Ofisi ya Rais mjini
Ouagadogou. Jeshilimezingira maeneo hayo Jumatano Jioni wiki hii.
Wanajeshi hao ni pamoja na wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa taasisi
mbalimbali za uongozi wa nchi (RSP), ambao waliingia wakati wa kikao cha
Baraza la mawaziri. Wanajeshi hao wamewapokonya silaha askari waliokua
wakitoa ulinzi katika maeneo hayo, na kuwapokonya simu za mawaziri
waliokua nazo na baadaye walifunga lango la Ikulu.
Kwa sasa,
ni vigumu kujua nini kinaendelea ndani majengo hayo. Rais wa mpito,
Michel Kafando na Waziri Mkuu Isaac Zida na Mawaziri kadhaa wa
serikaliwako mikononi mwa wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa taasisi za
uongozi wa nchi. Hakuna madai hadi sasa ambayo yametolewa na kundi hili
la wanajeshi.
Mahusiano
si mazuri kati ya Waziri Mkuu Isaac Zida, kutoka jeshi, na wanajeshi wa
Kikosi cha usalama wa Rais. Migogoro mingi - mwezi Desemba, Februari na
Juni - ilitokea kati ya Isaac Zida marafiki zake wa zamani. Na
kuingilia kijeshi kwa wanajeshi hao kunakuja wakati ambapo Jumatatu wiki
hii, tume ya maridhiano na mageuzi iliyoteuliwa katika kipindi cha
mpito ilitoa ripoti yake, ambayo inataka hasa kuvunjwa kwa kikosi cha
usalama wa rais (RSP). Je, kuna uhusiano ya moja kwa moja kati ya
matukio haya? Kwa sasa, bado ni vigumu kusema kwani madai ya askari
wanawashikilia viongozi hao hayajulikani.
Kuingilia
huko kwa wanajeshi wa RSPpia kunakuja wiki chache kabla ya uchaguzi wa
rais na wabunge, uliyopangwa kufanyika Oktoba 11 kama sehemu ya mchakato
wa mpito, ambayo ilianza baada ya kuanguka kwa utawala wa Blaise
Compaoré, Oktoba 31 mwaka 2014, baada ya miaka 27 akiwa madarakani.
No comments:
Post a Comment