BAADHI ya wakazi wa mji wa Dodoma wameeleza masikitiko yao juu ya matusi na kashifa zinazotolewa na viongozi wa CCM dhidi ya wahasimu wao Chadema.
Hali
hiyo ilijitokeza juzi ambapo Makongoro Nyerere aliweka sera za CCM
pembeni na kuanza kutoa kashfa kwa wagombea wa vyama vya siasa hususani
Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa na mgombea Ubunge Benson
Kigaila.
Akihutubia
katika mkutano wa Kampeni wa mgombea ubunge CCM katika viwanja vya
Kikuyu Kusini, Makongoro badala ya kutangaza sera za chama chake alianza
kwa kashfa na kudai Ikulu hakuna makabuli hivyo Lowassa anaumwa na kuna
uwezekano akafia Ikulu.
Makongoro
akimnadi Anthon Mavunde, alitumia muda mwingi kutoa kashfa kwa wagombea
wa UKAWA huku akidai Lowassa asichaguliwe kuwa rais kwani afya yake
mbaya hivyo anaweza kutofanya majukumu yake.
Mbali
na hilo amesema Ikulu siyo wodi ya wagonjwa na sehemu ya makaburi hivyo
ni vyema mtu anayetakiwa kwenda Ikulu ni mtu mwenye nguvu.
“Mimi
sasa sitaki kuendelea kumsema Lowassa maana akifa watasema mimi ndiye
niliyemuua hata hivyo nawashangaa watu wa UKAWA wana roho ngumu sana
kutembea na mtu ambaye amechoka vile.
“Chadema
wanatakiwa kushitakiwa ni maajabu sana kuona na watu wasivyo na huruma
wanamtesa sana baba wa watu hata hawezi kuzungumza majukwaani na sera
anamwachia Lissu (Tundu),” amesema Makongoro.
Kutokana na hali hiyo wakazi wa Dodoma wamesema watanzania wanataka kusikiliza sera na siyo vinginevyo.
Mmoja
wa wananchi wa Kikuyu Kaskazini ambaye alijitambulisha kuwa ni kada wa
CCM na kukataa jina lake litajwe alisema ana mashaka na wana CCM huenda
wana mpango wa kuua chama.
Alisema
haiwezekani viongozi wa CCM badala ya kutangaza sera wao wanajielekeza
katika matusi na kashifa,mambo ya afya ya mtu anaijua Mungu mwenyewe.