Mungu
huyo wa mdogo wa kiume mwenye daraja kubwa anayejulikana kwa zaidi ya
majina 125 (Ganpati Bappa Morya) mwenye sura ya tembo akiwa amewekwa
juu ya gari maalumu wakipita mitaa kadhaa ya jiji la Dar es Salaam leo
mchana akipelekwa Baharini ili kuungana na mungu wa kike waliopo kwenye
mito mitatu mikubwa mitakatifu iliyopo nchini India.
Mungu huyo akiwa amewekwa juu ya paa la gari akiwa katika uangalizi wa heshima.
Wanawake wa madhehebu hayo ya kihindu wakicheza wakati wa kuadhimisho siku hiyo.
Hapa ni furaha tupu ya maadhimisho hayo.
Hapa
wazazi na watoto wakiwa kwenye maandamano hayo kuelekea baharini
kumuweka ili kuungana na mungu wengine wa kike waliopo katika mito
mitatu mitakatifu iliyopo nchini India.
Maandamano yakiendelea.
Hapa ni furaha tupu kwa wanawake, wanaume, wazee na watoto.
Watoto wakifurahia maadhimisho hayo.
Hapa wakiwa juu ya magari kuelekea kumsindikiza mungu wao huyo.
Hapa wakiwa kwenye magari kuelekea baharini.
Ni furaha tupu ndani ya gari.
Safari ya kwenda baharini ikiendelea.
WATANZANIA
wenye asili ya India wa dhehebu la Hindu (Baniani), leo wameadhimisha
siku ya kuzaliwa kwa Mungu wa mdogo wa kiume mwenye daraja kubwa
(Ganpati Bappa Morya) na mwenye sura ya tembo.
Mungu
huyo hufanyiwa sherehe baada ya kufanyika kwa ibada ya siku tisa ambapo
siku yake ya kuzaliwa alipelekwa baharini kwaajili ya kuungana na Mungu
wa kike walio kwenye mito mitatu mitakatifu iliyopo nchini India ambayo
ni Sarasgad, Amba na Raigad.
Sherehe
hizo zilianza kwa ibada ambapo pia walitumia fursa hiyo kuiombea amani
ya nchi hii katika maadhimisho ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa
iliambatana na utoaji wa sadaka za vyakula mbalimbali na maombi
hupelekwa baharini kwa ajili ya kuungana na Mungu kike.
Katika
sherehe hizo jijini hapa zilianzia katika nyumba zao za ibada ambapo
kulikuwa na msafara mkubwa ambao ulihusisha na magari yaliyobeba Mungu
huyo huku wanawake wakijipamba kwa mavazi mazuri huku wakitembea na
kucheza kwa furaha kumsindikiza wakipita barabara kadhaa za katikati ya
jiji la Dar es Salaam zikiwemo za Azikiwe na Kivukoni hadi Baharini.
Baada
ya kufanyika kwa sherehe hizo pia baada ya miezi miwili kutakuwa na
maadhimisho ya mwaka mpya ambao ni Diwali ambapo mwaka ujao
wataadhimisha tena sherehe hizo.
Mungu
huyo ambaye pia hujulikana kwa majina zaidi ya 125 na ndiye Mungu mdogo
na mwenye daraja kubwa zaidi.Baadhi ya majina hayo ni Ganesh Chaturthi,
Vinayaka Chaturthi
Inaaminika
kuwa unapoomba kitu chochote kutoka kwake unafanikiwa. Ambapo mungu
huyo ambaye ni mwanaume aliyetengenezwa kwa aina ya udongo maalumu
huyeyuka anapowekwa baharini ikiwa na maana ya kwenda kuungana na Mungu
wa kike waliokatika mito hiyo.