Rais wa Urusi, Vladmir Putin
Rais wa Urusi,Vladmir Putin ametoa wito wa kuwepo kwa mpango wa kikanda wa kupambana na wanamgambo wa Islamic State.
Putin
amemuhakikishia kumuunga mkono Rais wa Syria, Bashar al-Assad,ambaye
mataifa ya magharibi na upinzani nchini Syria wamemtaka aondoke
madarakani.
Mzozo wa
Syria unatarajiwa kuwa miongoni mwa ajenda zinazotazamwa kwa karibu
zaidi wakati Viongozi wa dunia wanapokutana katika mkutano wa Umoja wa
Mataifa,jijini New York nchini Marekani.
Waziri Mkuu wa Uingereza,David Cameron anatarajiwa kulegeza msimamo wake dhidi ya Assad katika hotuba yake wiki hii.
Cameron
sambamba na Rais wa Marekani, Barrack Obama na rais wa Ufaransa,
Francois Hollande walikuwa wakimtaka rais Assad aondolewe madarakani ili
kuleta amani Syria, msimamo ambao umekuwa ukipingwa na Putin.
Kukutana
kwa viongozi wa Ulaya kunazidisha wito wa kuwepo kwa msukumo wa
kidiplomasia nchini Syria wakati huu ambapo kumekuwepo na wimbi la
wakimbizi wanaoelekea Ulaya.