Na RFI
Mawaziri
wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya wanapanga kukutana Jumanne ijayo,
Septemba 22 mjini Brussels kwa mkutano mwingine maalum juu ya suala la
mgogoro wa wakimbizi.
Ujerumani,
ambayo pamoja na Austria inayotoa wito wa kuandaliwa kwa mkutano wa
dharura wa Umoja wa Ulaya juu ya suala hili, imetuhumiwa kuendesha sera
"isiyoeleweka" , kwa kufuta sheria za Schengen. Angela Merkel amejitetea
kufuatia tuhuma hizo na ametaka kuwepo na mshikamano wa Ulaya.
Ujerumani
sasa inajiandaa kupokea kati ya watu 800,000 na milioni moja
wanaotafuta hifadhi. Tangu kuanza kwa mgogoro huyo, Berlin imezilaumu
nchi za Makedonia na Hungary kwa jitihada zao za kuwazuia wakimbizi,
akieleza kuwa nchi hizo zinatakiwa kuwapokea wakimbizi wote, na kwamba
Ujerumani iko tayari kupokea mamia ya maelfu.
Hivi
karibuni, Ujerumani ilionekana kurejelea kauli yake, kwa kuweka
utaratibu wa udhibiti kwenye mipaka yake na nchi jirani hasa Austria.
Hali hiyo imesababisha Ujerumani kukosolewa na waziri wa mambo ya ndani
wa Jamhuri ya Czech, na kutaja kuwa sera ya Ujerumani " haieleweki ".
Kansela Angela Merkel amesema kuwa kusimamishwa kwa Mkataba wa Schengen
lazima tu utarahisisha zoezi la kuurodhesha wakimbizi, lakini mtazamo wa
uamuzi huu ni tofauti , ukiangaliwa kiundani.
Mtazamo
wa Berlin, sera ya Ujerumani hata hivyo iko wazi na ni yenye kueleweka,
kama alivyobaini Kansela mwenyewe, inatakiwa "kurejelea msimamo wa
Ulaya" ili kufikia mgawanyo sawa wa wakimbizi miongoni mwa nchi
wanachama wa Umoja wa Ulaya, na kuandaa utaratibu wa kudhibiti wimbi la
wakimbizi wanaoingia barani Ulaya.
No comments:
Post a Comment