Hatua ya akaunti moja inalenga kupambana na vitendo vya udanganyifu
Muda
uliotolewa kwa wizara za Serikali ya Nigeria kuhakikisha kuwa michakato
ya huduma za kibenki zinafanyika kupitia akaunti moja ya Benki umefikia
tamati.
Hatua hiyo imefikiwa ili kurahisisha ufuatiliaji wa mienendo ya matumizi ya Serikali ili kupambana na vitendo vya rushwa.
Akaunti
hiyo itaratibiwa na Benki kuu ya nchini humo na inakadiriwa kuwa Benki
za biashara zitapoteza kiasi cha dola bilioni kumi pesa
zitakapohamishwa.
Wizara zitazoshindwa kutimiza agizo hilo zitawekewa vikwazo.
Rais
Muhamadu Buhari, aliyetoa agizo la kufunga akaunti mbalimbali za benki
amesema anaamini maafisa wa serikali wameiba kiasi cha dola bilioni 150
kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Naibu
Gavana wa Benki kuu ya Nigeria,Obadiah Mailafia ameiambia BBC kuwa
ilikuwa rahisi udanganyifu kufanyika kwa sababu Serikali haikujua kila
wizara ina akaunti ngapi za benki.
Mwandishi
wa BBC jijini Abuja amesema utekelezaji wa hatua ya ''akaunti moja''
umewezesha jimbo la kaduna kubaini kiasi cha dola milioni 13 ambazo
awali zilikuwa hazifahamiki kama zilikuwepo.BBC
No comments:
Post a Comment