Picha ya pamoja wakati viongozi hao walipotembelea TaTEDO.
Viongozi
wa taasisi za vijana kutoka kwenye nchini sita wamekutana mjini
Bagamoyo kujadili na kuandaa mtaala utakaotumika kuwafundisha vijana
namna ya kufanya ujasiriamali usioathiri mazingira “Green
Entrepreneurship”.
Mkutano
huo ambao ulitanguliwa na ziara ya mafunzo kwenye Shirika la Maendeleo
ya Nishati Mbadala (TaTEDO), umewashirikisha viongozi wa taasisi za
vijana kutoka Slovenia, Italia, Nepal, Ureno, Argentina na wenyeji
Tanzania walipata fursa ya kujifunza namna ya uzalishaji wa nishati
mbadala isiyoathiri mazingira.
Shukuru Meena, Mratibu wa miradi ya nishati kwenye Shirika la Maendeleo ya Nishati Mbadala (TaTEDO).
Chris
Ndallo (kushoto), Mtendaji Mkuu wa shirika la Maendeleo ya Vijana TYCEN
akijadiliana jambo na baadhi ya watumishi wa TaTEDO.
Viongozi wa taasisi za vijana, wakitazama baadhi ya miradi inayoendeshwa na TaTEDO wakati walipotembelea ofisi za shirika hilo.
No comments:
Post a Comment