Ofisa
Mtendaji Kata ya Temeke, Elias Wawa akizungumza katika uzinduzi wa awamu
ya pili kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake masokoni
uliofanyika soko la Temeke Sterio Dar es Salaam jana. Uzinduzi huo upo
chini ya mradi wa Mpe Riziki si Matusi ‘Acha Lugha Chafu na
Udhalilishaji Sokoni’ Unaendeshwa na Shirika Equality for Growth (EfG).
Mwenyekiti wa Mtaa wa Matumbi uliopo katika wilaya ya Temeke, Khatibu Lindi, akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Soko la Temeke Sterio, Hamad Juma Mtemi, akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Temeke, Agnes Soso, akizungumza katika uzinduzi huo.
Ofisa
Ufuatiliaji na Tathimini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Samora
Julius (kulia), akitoa mada mbalimbali kuhusu ukatili wa jinsia
masokoni wakati wa uzinduzi huo.
Ofisa Mradi wa EfG, Susan Sitta, akielezea historia fupi ya
shirika hilo.
Mkazi wa Chamanzi, Husna Abdallah akielezea udhalilishaji wa jinsia katika masoko.
Maofisa wa EfG wa ndani na nje ya nchi na wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mkutano ukiendelea.
Wananchi wakifuatila matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo.
Soko la Temeke Sterio ulipofanyika uzinduzi huo.
Taswira katika uzinduzi huo.
Msanii wa Kundi la Utamaduni la Machozi, akitoa burudani.
Burudani zikiendelea kutoka kundi la Machozi.
OFISA
Mtendaji wa Kata ya Temeke, Elias Wawa amelipongeza Shirika la Equality
for Growth (EfG), kwa jitihada zake na kupunguza ukatili wa kijinsia
dhidi ya wanawake masokoni.
Wawa
alitoa pongezi hizo Dar es Salaam jana, wakati akizungumza na wanahabari
katika uzinduzi wa awamu ya pili ya kupinga vitendo vya ukatili wa
jinsia dhidi ya wanawake katika Soko la Temeke Sterio.
“Nalipongeza
shirika la EfG kwa jitihada zao za kutoa elimu kwa wananchi katika
masoko mbalimbali kwani imesaidia kupunguza vitendo vya udhalilishaji na
ukatili wa jinsia masokoni” alisema Wawa.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Ofisa Mradi wa Shirika la EfG, Susan Sitta alisema
shirika hilo lililosajiriwa Septemba 6, 2015 dhima yake ni kuinua
maendeleo ya sekta isiyo rasmi Tanzania, hususani wanawake, kwa
kupunguza umaskini kwa njia ya kutoa mafunzo ya sheria na haki za
binadamu, kutoa msaada wa kisheria, kuwezesha kuwepo kwa fursa za
biashara kwa wanawake na wanaume pamoja na kushawishi utungaji wa sera
zinazoinua wanawake na kujenga uwezo sawa kwa wanawake na wanaume.
Sitta
alisema shirika hilo linatekeleza mradi unaoitwa Mpe Riziki si Matusi
katika masoko sita Wilayani Ilala ambayo ameyataja kuwa ni Feri, Kisutu,
Mchikichini, Gezaulole, Tabata Muslimu na Temeke Sterio.
Alisema
mradi huo umelenga kuwalinda wanawake katika sekta isiyo rasmi hususani
wafanyabiashara masokoni dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Aliongeza
kuwa mradi huo pia unaangalia wanawake wafanyabiashara katika masoko ya
ya Wilaya ya Ilala na Temeke na kuhakikisha wanafanyabiashara zao
katika mazingira huru yasiyo na ukatili wa matusi, kingono, kimwili,
kiuchumi na kisiasa.
“Mradi huu zaidi unaangalia na kuhakikisha wanawake wanaheshiwa na kufurahi haki yao ya kiuchumi” alisema Sitta.
Sitta
alisema utafiti uliofanywa na shirika hilo juu ya ukatili dhidi ya
wanawake masokoni unaonesha asilimia 90.32 ya wanawake katika sekta
isiyo rasmi wanafanyiwa ukatili mara kwa mara wa kingono, kimwili na
matusi katika maeneo yao ya kazi.
Mkazi
wa Chamanzi, Husna Abdallah alisema kufanyiwa viendo vya ukatili wa
jinsia kwa wanawake wafanyabiashara masokono kwa upande mwingine
kunachangiwa na wanawake wenyewe pale wateja wanapowashika katika miili
yao na wao kufurahi jambo hilo bila kuchukua hatua ya kuwakalipia au
kuwapeleka kwa uongozi wa soko husika.
No comments:
Post a Comment