KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka amesema anamshangaa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye kusaidia kampeni mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa.
Amesema
uamuzi huo wa Sumaye ni sawa na pwagu kumfanyia kampeni pwaguzi. Shaka
alitoa matamshi hayo jana katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa
kampeni za ubunge na madiwani jimbo la Mtwara Vijijini wakati akimnadi
mgombea wa jimbo hilo kupitia CCM, Hawa Ghasia.
Mkutano huo wa kampeni ulifanyika katika kijiji cha Mo Pacha Nne mkoani hapa.
Alisema
ni kituko kwa viongozi hao, ambao waliwahi kuwa viongozi wa juu wa
serikali ya CCM na kushindwa kuleta ufanisi na matokeo chanya, sasa
wakiwa Chadema kughilibu wananchi wakidai wana ubavu wa kuleta
mabadiliko na maendeleo.
“Sumaye
anapomfanyia kampeni Lowassa awe Rais ni sawa na pwagu kumfanyia
kampeni pwaguzi, hawajui wafanyalo, hawatambui kama majina yao
hayaheshimiki mbele ya jamii, walipewa nafasi za juu wakashindwa
kuisukuma nchi kimaendeleo,” alisema Shaka.
Alisema
Sumaye akiwa Waziri Mkuu wa Serikali chini ya awamu ya tatu ya Rais
Benjamni Mkapa, usimamizi wake alisababisha halmashauri nyingi za wilaya
nchini kupata hati chafu kwa mujibu wa ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Aidha,
Shaka alifichua siri ya jina la Lowassa kukatwa na vikao vya CCM katika
mbio za urais, huku akisema halikuwa jambo la bahati mbaya.
No comments:
Post a Comment