KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba amewaasa Watanzania kutofanya makosa kwa kumchagua Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa kuwa Rais wa Tanzania na badala yake wamchague Dk John Magufuli ambaye ni kiongozi makini anayejali shida za wananchi.
Akizindua
kampeni za Jimbo la Mtera Kijiji cha Nagulo Kata ya Mpwayungu, Makamba
alisema Dk Magufuli ni kiongozi anayekerwa na matatizo ya watu na
kuyatatua.
Makamba
alidai kuwa mgombea wa Chadema anadai kukerwa na matatizo ya watu,
lakini wakati akiwa Waziri wa Ardhi alipora Ranchi ya Mzeli na kuifanya
yake na familia yake.
Alisema
hakuna zawadi nzuri, itakayoonyesha shukrani kwa Rais Jakaya Kikwete
kwa mema aliyoyafanya katika uongozi wake, zaidi ya kuchagua viongozi
wanaotokana na CCM kuanzia nafasi ya urais, ubunge na udiwani.
“Livingstone
Lusinde nimemlea mwenyewe, najua utendaji wake wa kazi na jimbo la
Mtera limesikika na kupata umaarufu kwa sababu yake, hivyo ni vyema
mkamchagua tena ili aendeleze na kumaliza yale aliyoyaanza,” alisema.
Kwa
upande wake, Lusinde aliwataka viongozi wa dini waiombee nchi ili
uchaguzi ufanyike kwa amani na kutoa mwito kwa viongozi wote dini nchini
kuomba ili uchaguzi umalizike kwa amani na Rais bora apatikane.
No comments:
Post a Comment