Mgeni
rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues (wa pili kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja
wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan mara baada ya
kuwasili kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Nyanza jijini Mwanza kwenye
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani ambapo kitaifa yamefanyika
jijini humo na kuandaliwa na Baraza la Dini mbalimbali la Amani Tanzania
(IRCPT) kwa ushirikiano wa UNESCO ambapo yaliwashirikisha Viongozi wa
Serikali, Asasi za Kiraia, Waandishi wa habari, Viongozi wa madhehebu ya
dini, Jeshi la Polisi, Walemavu, Wananchi pamoja na Ofisi ya Msajili wa
vyama vya siasa. Kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji
Francis Mutungi na wa pili kulia ni Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa
vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia.
Umoja wa
Mataifa (UN) umesema utaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania
kulinda na kudumisha amani ya pamoja kwa makundi yote ili amani iliyopo
itumike kuleta maendeleo endelevu nchini.
Hayo
yamebainishwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),
Zulmira Rodrigues, wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya
siku ya Amani Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza (Septemba
21.2015).
Bi.Rodgrigues
amesema amani ya pamoja inatoa nafasi kwa kila mmoja kuwa mshirika wa
kudumisha na kuendeleza amani bila kujali itikadi, imani au matabaka
mbalimbali yaliyipo ndani ya jamii.
Amefafanua
kuwa Tanzania ni mfano wa kuigwa katika kulinda amani, hivyo nguvu ya
pamoja ni muhimu katika kufikia malengo na maendeleo yanayotakiwa
kutokana na kuwepo kwa utulivu, mshikamano, umoja, na amani.
Kwa
upande wake, Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi
amewataka watanzania kuachana na propaganda za kisiasa zinazoleta chuki
na hasa katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Jaji
Mutungi ameeleza kuwa amani haina tabaka na kusisitiza umuhimu wa
wananchi kupiga kura kwa kutumia falsafa ya kulipenda taifa na kuwaonya
viongozi wa vyama vya siasa kuacha kuwadharau watanzania ambao
wameilinda amani kwa muda mrefu.(P.T)
Nalo
Jeshi la Polisi mkoani humo, limelaani kitendo kilichofanywa na watu
wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa vyama vya siasa kwa kushambulia polisi
na kuvunja vioo vya gari la polisi kwa kusingizio cha kampeni za
uchaguzi.
Katika
tukio hilo imeelezwa kuwa, baada ya watu waliokuwa wakitokea katika
mkutano wa kampeni wa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) kushambulia
Polisi, kuvunja vioo vya gari la polisi na kujeruhi askari.
Mkuu wa
wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga akisoma hotuba kwa niaba ya Kaimu
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kwenye maadhimsho ya siku ya
kimataifa ya Amani Duniani ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo
ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika
kilele hicho cha siku ya Amani jijini hapa.
Kamanda
Mkumbo ameeleza kuwa kitendo hicho ni uhalifu kama uhalifu mwingine na
polisi haiwezi kuvumilia vitendo vya aina hiyo na hasa wakati huu ambapo
kampeni za uchaguzi zinaendelea.
Maadhimisho
ya siku ya amani duniani yanafanyika septemba 21, kila mwaka ili
kukumbuka na kulinda amani na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Amani Kwanza –
Utamaduni wetu wa amani ni nguvu yetu”. Ambapo siku hiyo pia viongozi
mbalimbali waliweza kuhudhuria siku hiyo wakiwemo viongozi wa siasa,
dini, jeshi la Polisi, viongozi wa serikali na binafsi pamoja na
wananchi mbalimbali.
Mkuu wa
Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akitoa ujumbe
maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Unesco, Irina Bokova kwenye sherehe
za maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Amani Duniani ambayo kitaifa
imefanyika jijini Mwanza.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo
akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Amani
Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
Msajili
wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi akitoa nasaha zake
kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani Duniani ambapo kitaifa
yamefanyika jijini Mwanza.
Jukwaa
kuu la viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku
ya Kimataifa ya Amani ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo
akiteta jambo na Mgeni rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),
Zulmira Rodrigues wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa
ya Amani, ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
Kikundi cha kwaya ya Patimo-Mabatini jijini Mwanza kikitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
Burudani ya Qaswida maalum iliyobeba ujumbe wa kutunza 'Amani' ikitolewa.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Baraka Konisaga akiweka saini kwenye Azimio
maalum la kuenzi Amani lililoandaliwa kwenye maadhimisho hayo huku Mgeni
rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Dini mbalimbali
la Amani Tanzania (IRCPT), Rev. Canon Godda (wa pili kulia) wakishuhudia
tukio hilo.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo
(kushoto) na viongozi mbalimbali wa dini wakiendelea kusaini Azimio
hilo.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues akiweka sahihi kama shuhuda katika kupitisha Azimio hilo.
Msajili
wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi naye akiweka saini kama
shuhuda wa kupitisha Azimio hilo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, Baraka Konisaga.
Pichani
juu na chini ni makundi ya Viongozi mbalimbali wa madhehebu ya dini,
Viongozi wa Serikali, Asasi za Kiraia, Waandishi wa habari, Jeshi la
Polisi na Walemavu waliodhuruia siku ya Kimataifa ya Amani Duniani
ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza katika viwanja vya Shule ya
msingi Nyanza.
Wawakilishi wa vikundi vya vijana walioshiriki maadhimisho ya siku ya Amani Duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mwanza.
Baadhi ya
wanafunzi wa Shule ya msingi Nyanza walikuwa ni miongoni mwa washiriki
wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani duniani.
Meza kuu katika picha ya pamoja.
Washiriki katika picha ya pamoja na meza kuu.