MUUMIN MWINYJUMA NA DOUBLE O WAANZA MAONYESHO MSUMBIJI - LEKULE

Breaking

22 Sept 2015

MUUMIN MWINYJUMA NA DOUBLE O WAANZA MAONYESHO MSUMBIJI


KUNDI  la Double M chini ya Muumin Mwinyjuma, limealikwa Msumbiji kwa mwezi mzima, na katika wakati huo kundi litashiriki katika sherehe za miaka 51 ya Vita vya Ukombozi wa nchi hiyo. Wanamuziki hawa ambao ni wanachama wa Mtandao wa Wanamuziki walipitisha barua yao ya taarifa ya kwenda huko na hivyo Mtandao ukatoa taarifa Baraza la sanaa La Taifa kama inavyostahili. Waliomo katika msafara huo ni pamoja na kiongozi wa kundi Muumin Mwinyjuma,  maarufu kwa jina la KOCHA, na wanamuziki wengine 16.
Mwinjuma Muumin Buguza- Kiongozi wa Bendi-Muimbaji, Omary Kisila- Kinanda,  Hamza S Waninga- Drums, Imma Keffa –Bass Guitar, Emmanuel Namwinga- Rhythm guitar, Amina R Juma –Muimbaji, Veronica D Buzeri –Dansa, Neema Kawambwa-Dansa, Stamili  Hamis –Dansa, Greyson Semsekwa – Rapper, Sharey Aboubakar-Muimbaji, Revina Mzinja -Dansa, Salma Shaaban –Dansa, Afande Muhamada-Fundi Mitambo, Omary Maulid –Fundi Mitambo, Saleh Kupaza-Muimbaji, Dogo Rama-Muimbaji.
Habari toka TAMUNET- Mtandano wa Wanamuziki Tanzania