Mwakilishi
wa Kampuni ya Uchimbaji wa Visima ya ZENTAS kutoka Uturuki nchini
Tanzania Dkt, Mohammed Akbar akitoa taarifa za kukamilika kwa kazi ya
uchimbaji wa kisima chenye urefu wa mita 541 eneo la Mkwalia, Mkuranga,
Pwani leo.Kisima hicho kinauwezo wa kuzalisha maji lita milioni 1.8 kwa
siku.
Maji kutoka katika kisima hicho yakitiririka kufuatia kufanyika kwa majaribio ya kuyatoa maji kutoka ardhini.
Kiongozi
wa waendesha mitambo ya uchimbaji visima wa kampuni ya ZENTAS Bw. Sima
Teodor ( kushoto) akitoa maelezo kwa wandishi wa habari kuhusu kazi ya
uchimbaji wa kisima hicho katika eneo la mradi wilayani Mkuranga.
Msimamizi
wa mradi huo kutokaKampuni ya ZENTAS, Muhandisi Lami
Karagoz (katikati) akifafanua teknolojia na vifaa vilivyotumika kuchimba
kisima hicho.(Picha na Aron Msigwa/ MAELEZO).
Na
Aron Msigwa- MAELEZO Mkuranga, PwaniWananchi wa wilaya ya Mkuranga,mkoa
wa Pwani wanatarajia kunufaika na mradi mkubwa wa usambazaji wa maji
kufuatia kukamilika kwa zoezi la uchimbaji wa kisima cha maji chenye
urefu wa mita 541 ambacho kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 1.8 kwa
siku.Akitoa taarifa za kukamilika kwa kazi ya uchimbaji wa kisima
hicho mwakilishi wa kampuni ya kuchimba visima ya ZENTAS kutoka
Uturuki nchini Tanzania Dkt.Mohammed Akbar amesema wao kama wataalam
wanaendelea na majaribio ya kuyatoa maji kutoka ardhini jambo ambalo
limeonyesha mafanikio makubwa. Amesema mtambo wa kuchimba kisima hicho
uliwasili eneo la mradi Julai 9 mwaka huu na kuongeza kuwa mara baada ya
kuwasili katika eneo la mradi kazi ya uchimbaji ilianza na kubainisha
kuwa sasa kisima hicho kinazalisha kiasi cha lita 76,000 kwa saa na
lita milioni 1.8 kwa siku.Dkt. Akbar amesema endapo maji hayo
yataunganishwa kwenye miundombinu ya maji ya mji huo yatakidhi mahitaji
ya maji ya mji wa Mkuranga ambayo ni lita laki Sita na Elfu mbili kwa
siku (602,000).” Kwetu Haya ni mafanikio makubwa ukizingatia mradi
wenyewe haujaanza kusambaza maji kwani visima hivi vilikuwa ni kwa ajili
ya utafiti, kiwango cha maji kilichopatikana ni kikubwa, kilichobakia
sasa ni kwa mamlaka husika na Serikali kukamilisha mipango iliyobaki ili
maji haya yawafikie wananchi” Amesema.Ameongeza kuwa chini ya mradi huo
wamechimba visima 9 na kati ya hivyo visima 7 vinafanya vizuri na 2
vimeharibika na kueleza kuwa matarajio yao ni kuona visima vitano
ambavyo sasa vimekamilika vizuri vikizalisha lita milioni 55.Meneja wa
Mamlaka ya Maji Mkuranga mjini (MKUWASA) Muhandisi Filbert Pius
akiuzungumzia mradi huo amesema kuwa utakapokamilika utawasaidia
wananchi kupata maji safi na kuondoa tatizo la muda mrefu la ukosefu wa
maji katika maeneo mbalimbali ya mji huo.Amesema mahitaji ya maji katika
mji huo ni makubwa kuliko uwezo wa sasa wa kuzalisha maji ambapo vyanzo
vilivyopo vina uwezo wa kuzalisha lita 135,000 kwa siku ikilinganishwa
na mahitaji ya sasa ya lita 602,000 kwa siku kwa wakazi wapatao
25,847.Ameiomba Serikali kuendelea kutoa fedha za kufanikisha ujenzi wa
miundombinu yenye urefu wa kilometa 2 inayotarajiwa kukamilika ndani ya
mwezi huu ili Mkuranga ambao sasa ni mji wa viwanda upate huduma ya
uhakika ya maji.Pia amesema kukamilika kwa ujenzi wa matenki makubwa ya
kuhifadhia maji eneo la Mkwalia ulipo mradi huo pamoja na eneo la
Kurungu kutaiwezesha hospitali ya Wilaya ya Mkuranga kupata huduma ya
uhakika ya maji ambayo imekuwa kero ya muda mrefu kwa wagonjwa wanafika
kupata huduma.Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji
Taka (DAWASA) Bi.Nelly Msuya akifafanua kuhudsu mradi huo amesema
unajengwa unatekelezwa na DAWASA kwa niaba ya Serikali na akifafanua
kuwa maeneo yote yenye miundombinu ya maji katika wilaya ya Mkuranga
yanatarajiwa kuanza kupata huduma hiyo ifikapo Oktoba mwaka huu.Amesema
mradi huo sasa uko katika hatua za majaribio na unatarajiwa kuwanufaisha
wananchi wote mara kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu kwenye maeneo
ambayo hayakuwa na mabomba ya kusambazia maji , ujenzi wa matenki
makubwa ya kuhifadhia maji na kukamilika kwa taratibu za kitaalam ili
maji hayo yawafikie wananchi.“Nachoweza kusema kwa upande wa wilayanya
Mkuranga tumefika pazuri, sisi kama DAWASA watekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maji kwa niaba ya Serikali tutahakikisha kero ya maji
katika wilaya hii na maeneo mengine inapatiwa ufumbuzi, tumeshatoa
mamlaka kwa miji na wilaya kubuni, kusimamia na kuendeleza miradi ya
maji ili wananchi wengi zaidi wanufaike” Amesisitiza.Aidha, amebainisha
kuwa mradi wa ujenzi wa visima 8 eneo la Mkuranga umegharimu kiasi cha
shilingi bilioni 7.4 na kufafanua kuwa awamu inayofuata ni kuyapeleka
maji hayo yakaunganishwe na mfumo wa kusambazia maji uliopo, ujenzi,
uongezaji wa matenki makubwa ya kuhifadhia maji na ununuzi wa pampu ya
kusukuma maji hayo kutoka kwenye chanzo.
No comments:
Post a Comment