BARNABA AZUSHIWA KUJIINGIZA KWENYE INJILI - LEKULE

Breaking

17 Sept 2015

BARNABA AZUSHIWA KUJIINGIZA KWENYE INJILI


Staa wa muziki wa Bongo Fleva kutoka Jumba la Vipaji (THT), Barnabas Elius a.k.a Barnaba.
Boniphace Ngumije
STAA wa muziki wa Bongo Fleva kutoka Jumba la Vipaji (THT), Barnabas Elius a.k.a Barnaba hivi karibuni alizushiwa na baadhi ya watu wakiwemo marafiki zake wa karibu kuwa amejiingiza kwenye uimbaji wa nyimbo za Injili jambo ambalo amelikanusha vikali.

Akichonga na Centre Spread, Barnaba alisema taarifa hizo za yeye kujiingiza kwenye muziki wa Injili aliziona kwenye mitandao ya kijamii na kuzisikia kutoka kwa baadhi ya watu wake wa karibu lakini anashindwa kuzielewa zilianzia wapi.
“Sijawahi kusema kuwa najihusisha na Injili wala kuwa nina mpango wa kujihusisha, inanishangaza sana kusikia taarifa hizo lakini nakumbuka nilichosema ni kwamba hivi karibuni nitatoka na albamu yangu mpya ambayo bado sijaipa jina, itakayokuwa na nyimbo kumi, nne zikiwa za kuhamasisha na zilizobaki zitakuwa za kawaida tu,” alisema Barnaba.

No comments: