|
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda (kulia)
akimpokea Mfalme wa Lesotho, Mhe. Letsie III (kulia) alipowasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Mfalme Letsie
ambaye pia ni Kiongozi wa kuhamasisha masuala ya Chakula na Lishe wa
Umoja wa Afrika yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kwanza wa
Dunia kuhusu umuhimu wa kuongeza Virutubisho kwenye Chakula. Mkutano huo
unafanyika Jijini Arusha kuanzia leo tarehe 09 hadi 11 Septemba, 2015. |
|
Waziri
Mkuu Mhe. Pinda (katikati) akimtambulisha Mkurugenzi wa TANAPA Dkt.
Allan Kijazi (wa kwanza kulia) kwa Mfalme Letsie (wa kwanza kushoto). |
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo
Pinda (wa kwanza kulia) akimtambulisha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu
CCM Arusha Mhe. Catherine Magige (wa pili kutoka kushoto) kwa Mfalme
Letsie (wa pili kutoka kulia).
|
Mfalme Letsie akiwapingia Mkono moja ya vikundi vya ngoma vulivyokuwepo uwanjani hapo. |
|
Mhe. Pinda akimwongoza Mfalme Letsie III mara baada ya kumpokea. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Daudi Felix Ntibenda. |
|
Mhe.
Waziri Mkuu kwa pamoja na Mfalme Letsie III wakiwa wameongozana pamoja
na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Ntibenda na Mkurugenzi Msaidizi, Idara
ya Itifaki katika Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bw. James Bwana (mwenye tai nyeupe).
Mhe. Pinda akizungumza na Mfalme Letsie mara tuu baada ya kuwasili uwanjani hapo.
Tanzania imekuwa mwenyeji wa
Mkutano wa Kwanza wa Dunia kuhusu umuhimu wa kuongeza Virutubisho kwenye
Chakula kwa ajili ya Lishe Bora utakaofanyika kwa siku tatu Jijini
Arusha kuanzia tarehe 09 hadi 11 Septemba, 2015.
Mkutano huo ambao utahudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda, utafunguliwa rasmi na Mfalme wa
Lesotho Letsie III ambaye ni Kiongozi wa kuhamasisha Lishe na Chakula
Bora wa Umoja wa Afrika.
Mkutano huo ambao ni wa kwanza
kufanyika, utajadili masuala mbalimbali yanayohusu umuhimu wa kuongeza
virutubisho kwenye chakula ikiwemo vitamini na madini muhimu ili
kuwawezesha watu duniani kote kuwa na afya bora kwa ajili ya uzalishaji
na kuleta maendeleo na hatimaye kuondokana na umaskini.
Pia Mkutano huu ni sehemu ya
jitihada za kimataifa katika kukomesha lishe duni na utapiamlo
uliokithiri katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.
Aidha, Mkutano huo
utawashirikisha wadau na wataalam mbalimbali kutoka Mashirika ya
Kimataifa, Sekta Binafsi na Serikalini. Mashirika hayo ni pamoja na
Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Afya
Duniani (WHO), Shirika la Chakula Duniani (WFP) na Umoja wa Afrika
(AU).
Mkutano huo umeandaliwa na
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Taasisi ya Global
Alliance for Improved Nutrition (GAIN) ya Uingereza. |
No comments:
Post a Comment