Rais
François Hollande na Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron katika
mkutano wa G7 Juni 7, 2015 katika mji wa Garmisch-Partenkirchen.
Na RFI
Kutokana
na hatari ya mashambulizi yanayoongozwa kutoka Syria, Ufaransa na
Uingereza wamepania kuendesha mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la
Islamic State (IS) nchini humo, ambapo London imefanya shambulizi la
kwanza ikitumia ndege isio na rubani mwishoni mwa mwezi Agosti.
Ufaransa
itafanya tangu Jumanne wiki hii upelelezi juu ya anga ya Syria," amesema
Rais François Hollande Jumatatu wiki hii katika mkutano wake mkuu wa
sita na waandishi wa habari. "Upelelezi huo utapelekea kuendesha
mashambulizi dhidi ya Daech, kwa kuhifadhi uhuru wetu wa utekelezaji na
uamuzi ", amesema rais wa Ufaransa.(P.T)
" Leo hii
nchini Syria, tunachotaka, ni kujua, kufahamu kinachoandaliwa dhidi
yetu na kile kinachofanywa dhidi ya watu wa Syria ", ameeleza Rais
Hollande, wakati ambapo Ulaya inayokabiliwa na ongezeko kubwa la
wahamiaji kutoka Syria, inmeendelea kukumbwa na mgogoro wake mbaya wa
uhamiaji tangu kumalizika kwa vita vikuu vya pili vya dunia.
Kwa upnde
wa Ufaransa, lengo ni kupunguza tishio la mashambulizi katika ardhi
yake. Mashambulizi yaliosababisha vifo dhidi gazeti la kila wiki la
Charlie Hebdo, shambulizi lililofanywa mwishoni mwa mwezi Agosti katika
treni ya mwendo wa kasi iliyokua ikisafiri kutoka Amsterdam kwenda Paris
(Thalys), shambulizi ambalo lilitibuka, yote hayo yana uhusiano na
itikadi kali za kidini na kundi la Islamic State lilikiri kutekeleza
baadhi ya mashambulizi.
Upelelezi
huo juu ya anga ya Syria utaruhusu Ufaransa kukusanya taarifa ambazo
ilishindwa kupata kuhusu vituo vya mafunzo na uamuzi wa kundi la Islamic
State nchini Syria.
London
Jumatatu ilitoa sababu ya usalama, ikieleza kuwa iliweza kutekeleza
shambulizi la anga nchini Syria Agost 21, shambulizi ambalo lililenga
ngome za kundi la Islamic State.
“
Wanajihadi watatu, ikiwa ni pamoja na Waingereza wawili, waliuawa katika
shambulizi lililoendesha kwa umakini na ndege isio na rubani ya RAF ",
Waziri mkuu David Cameron amewaambia wabunge.
" Ilibidi
tufanye hivyo kwa sababu watu hao walikuwa wakiajiri na kuandaa
mashambulizi ya kijinga dhidi ya nchi za Magharibi. Na kwa sababu katika
ukanda huo, hakuna serikali ambayo tunaweza kufanya ushirikiano ",
amesema David Cameron.
No comments:
Post a Comment