Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz, amemvaa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akimuita kuwa ni mtu mwongo, mbinafsi na mpotoshaji mkubwa.
Rostam
alieleza hayo katika taarifa yake jana kwa vyombo vya habari kuhusiana
na tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi yake jijini Dar es Salaam juzi,
alipozungumza na vyombo vya habari kuelezea mambo kadhaa zikiwamo
sababu za kujiondoa ndani ya Chadema.
Dk.
Slaa alidai kuwa mwaka 2009 baada ya kutaja orodha ya mafisadi 11
nchini katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mwembeyanga,
Dar es Salaam, Rostam alimpigia simu na kumtishia maisha.
Dk.
Slaa pia alidai juzi katika mkutano wake na vyombo vya habari
uliorushwa na vituo vitatu vya runinga kuwa Rostam anaifadhili Chadema.
Katika taarifa yake jana, Rostam alisema: “Nilimsikiliza
Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willibrod Slaa jana (juzi) alipokuwa
akizungumza katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
“Kwa
mara nyingine kama ilivyo hulka yake miaka yote, Dk. Slaa kathibitisha
pasipo na shaka kwamba yeye ni mbinafsi na mpotoshaji mkubwa.”
“Nimesikitishwa
na kushtushwa japo sikushangazwa hata kidogo na hatua ya Slaa ambaye
sasa anaonekana kukubuhu kwa uzushi kutoa matamshi ya namna hiyo.
"Sijapata
hata mara moja kuwa na mawasiliano na Dk Slaa wakati wowote. Madai yake
kwamba eti nilimtisha ni ya kupuuzwa na yasiyo na msingi hata kidogo,” alisema Rostam.
Rostam
alieleza kuwa ni jambo lisiloingia akilini hata kidogo kwa watu
wanaomfahamu Slaa kwamba anaweza kumtishia maisha na yeye akakaa kimya
bila kuchukua hatua ya kwenda polisi na kumshitaki halafu anakaa na
jambo hilo kwa miaka yote hadi juzi ndipo alisema hadharani.
“Ili kuthibitisha madai yake hayo, namtaka Dk. Slaa kujitokeza hadharani na kutoa ushahidi wa jambo hilo,” alisema Rostam.
Huu ni uongo mwingine wa dhahiri. Namtaka Dk. Slaa kutoa ushahidi pia katika madai yake haya.
“Ni
huyu huyu Dk. Slaa ambaye mwaka 2010 alizusha kwamba eti mimi, tukiwa
na Rais Jakaya Kikwete na Edward Lowassa tulikutana katika hoteli ya La
Kairo, Mwanza na kupanga njama za kumuibia kura zake za urais,” alisema na kuongeza:
“Wakati
Slaa akitoa madai hayo ya uongo, mimi nilithibitisha kwamba wakati huo
nilikuwa Afrika Kusini na Rais Kikwete akiwa Lindi huku Lowassa akiwa
Arusha. Ni wazi kwamba tusingeweza kukutana La Kairo kama alivyodai
yeye.”
Kwa
mujibu wa Rostam, Dk. Slaa kuna wakati alimzushia hadi Rais Kikwete
alipodai kwamba alisafiri kwa usiku mmoja kwenda China kumtoa mwanaye
aliyekuwa amekamatwa na vyombo vya usalama, kisha kurejea Dar es Salaam
usiku huo.
“Ni
Slaa huyu huyu ambaye mwaka 2010 wakati wa kampeni alifikia hatua ya
kuutangazia umma wa Watanzania kwamba kulikuwa na malori yaliyobeba kura
za CCM ambazo zingesaidia ushindi wa wizi yaliyokamatwa Tunduma. Malori
hayo yalipokaguliwa yalibainika kuwa na mizigo ya kawaida,” aliongeza katika taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment