Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete jana
jumanne amelihutubia kwa mara ya mwisho Baraza Kuu la 70 la Umoja wa
Mataifa akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hotuba
ya Mhe. Rais na ambayo iligusia mambo mengi ya kisiasa, kiuchumi, na
maendeleo akitumia pia fursa hiyo kuwaanga viongozi wenzie na
kuwashukuru kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi cha miaka kumi
ya uongozi wake, iliwasisimua wajumbe wa mkutano huo kiasi cha
kukatishwa mara kwa mara kwa makofi.
Zifuatazo ni baadhi ya picha
zinazomwonyesha Mhe. Rais katika Matukio mbalimbali Moja wapo likiwa
ni hafla ambayo Rais wa Marekani, Mhe Barack Obama aliiandaa kwaajili
wa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali waliohudhuria Mkutano wa 70 wa
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Picha kwa hisani ya Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
katika picha ya pamoja na Mhe.Barack Obama na Mkewe Michelle Obama
wakati wa hafla ilioandaliwa na Rais wa Marekani kwaajii ya Viongozi
wa Wakuu Nchi na Serikali wanaohudhuria Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la
Umoja wa Mataifa ( Picha hii ni kwa hisani ya Ofisi ya Itifaki ya
White House)
Mhe.
Rais Kikwete akiwa na Mhe. Sophia Simba, Katibu Mkuu Balozi Liberata
Mulamula na mwanamitindo Flaviana Matata muda mfupi mara baada ya
kulihutubia Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa
Mwakilishi
wa Kudumu wa Antigua na Bermuda Balozi Walton Alfonso Webson ambaye
ni mlemavu wa kutoona akimwongoza Mhe. Rais Kikwete kwenda kuonana na
Waziri Mkuu wake, Mhe. Gaston Alphoso Browne aliyekuwa na mazungumzo
wa Mhe.Rais mara baada ya Mhe. Rais kulihutubia Baraza Kuu la 70 la
Umoja wa Mataifa.
Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda Mhe. Gaston
Alphonso Browne, wengine katika mazungumzo hayo ni Mwakilishi wa Kudumu
wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi,
Mwakilishi wa kudumu wa Antigua na Barbuda, Balozi Walton Webson
mwenye miwani myeusi na Mkurungezi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa
Balozi Celestin Mushy