Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Wakati
shule zote za serikali na za binafsi nchini Kenya zikianza kufungwa
kuanzia hii leo, rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta akihutubia taifa hilo
kwa njia ya televisheni amesisitiza kuwa serikali yake haina uwezo wa
kulipa nyongeza ya mishahara wanayodai waalimu wanaoendelea na mgomo.
Mgomo wa walimu nchini Kenya
Ametoa
wito kuwa, mgogoro huo utatuliwe kwa amani na kusema kuwa shule zote
zinafungwa kuanzia leo. Serikali ya Kenya imeagiza shule zote nchini
humo zifungwe kuanzia leo huku mgomo wa walimu nchi nzima ukiendelea.
Barua
kutoka kwa wizara ya elimu imeagiza shule zote za serikali na za
kibinafsi zifungwe na wanafunzi warudi majumbani mwao. Watakaosalia
shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya
darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.