Jeneral Gilbert Diendere
Jenerali
Gilbert Diendere aliyefanya mapinduzi nchini Burkina Faso amesema kuwa
yupo tayari kukabidhi serikali kwa utawala wa kiraia kama
ilivyopendekezwa na wapatanishi.
Diendere
ambaye alipindua serikali hiyo siku ya alhamisi wiki iliyopita anasema
kuwa alifikia uamuzi huo kwa lengo la kile anachokiita kuepusha umwagaji
mkubwa wa damu.
Kauli yakekukiri kukabidhi madaraka inakuja huku majeshi ya serikali yaki ukaribia mji mkuu wa Ouagadougou
Jeshi la
Burkina Faso limeahidi kuwepo kwa hali ya Usalama kutokana na mapinduzi
hayo,japo kuwa wameahidi kuto waangamiza waliofanya mapinduzi hayo iwapo
tu watasalimisha silaha zao.
Hata hivyo kwa sasa Jeneral Diendere anadaiwa kujificha nyumbani kwa kiongozi wa kijadi Mogho Naaba.
Mamia ya watu wamezagaa mitaani katika mji mkuu wa nchi hiyo kwaajili ya kusherehekea.