Namelok Sokoine Azinduwa Kampeni Jimbo la Monduli…! - LEKULE

Breaking

30 Sept 2015

Namelok Sokoine Azinduwa Kampeni Jimbo la Monduli…!


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Namelok Sokoine akihutubia wananchi katika mkutano huo wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni zake.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Namelok Sokoine akihutubia wananchi katika mkutano huo wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni zake.
MGOMBEA jimbo la Monduli kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine, akihutubia mkutano wa hadhara wakati wa uzinduzi wa kampeni zake zilizofanyika katika viwanja vya Nanja Mnadani Monduli mkoani Arusha Septemba 28,2015 ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi
kuendeleza yote aliyoasisi, kusimamia na kutekeleza aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Edward Lowassa.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro akihutubia mkutano wa  uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine.
 Namelok Moringe Sokoine akiwasili katika uwanja huo wa Nanja tayari kwa uzinduzi wa kampeni.
Wazee wa Kimila wa Jamii ya Kimaasai wa Monduli wakiongoza dua maalim ya kumuombea Binti yao Namelok.
 Mwalimu Lorinyu Nkoosi, mmoja wa waliochuana na Namelok Sokoine katika mchakato wa uteuzi ndani ya CCM akiongea.
 Wananchi wa Monduli wakiwa katika mkutano huo.
Wajane wa Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine ambao ni mama za Namelok Sokine wakitambulishwa mkutanoni hapo na Mwenyekiti wa kamati ya kampeni za CCM jimbo la Monduli, Paul Kiteleki.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro (kulia) akimkabidhi ilani ya Chama cha Mapinduzi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine wakati wa uzinduzi wa jkampebni zake uliofanyika Monduli jana.

 Dk Asha-Rose Migiro akisalimiana na wamama wa kimaasai alipowasili mkutanoni hapo.