Kamishina
wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella
Bhalalusesa akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya
Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl.
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Na mwandishi wetu
JUMLA
ya wanafunzi 60,000 katika shule 150 nchini wamepitiwa na mafunzo ya
programu ya Bridge IT yenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kutumia
teknolojia ya kisasa ya kidijiti (digital technology) katika
ufundishaji na ujifunzaji wa Hisabati,Sayansi na Stadi za Maisha.
Hayo
yamsemwa na Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Profesa Eusella Bhalalusesa akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama.
Alisema
kutokana na mafanikio yaliyotokea sasa wanatanua wigo baada ya
kuwezeshwa kifedha na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya elimu (Global
Partnership For Education) kwa ajili ya kuendeleza teknolojia hiyo
katika kujifunza na kufundisha katika shule za msingi na hasa darasa la
awali la kwanza hadi la nne.
Aidha
maonesho hayo yanayofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere yana lengo la kuonesha ubunifu ambao upo tayari kutumika
kufanikisha mafunzo hayo.
Pia
maonesho hayo yanatarajia kujadili na kuangalia mbinu za kielektroniki
zitakazoweza kuendana na mazingira ya Tanzania katika ufundishaji na
kujifunza kwa gharama nafuu.
Pia wanatarajia kuangalia utayari wa walimu na namna ya kuwabadilisha mtazamo ili waweze kufundisha na kufundishika.
“Lengo
la serikali kupitia Wizara ya Elimu ni kupanua wigo wa elimu hasa elimu
ya awali kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano ambayo
itabadilisha ufundishaji kutoka kutumia vitabu vilivyopo katika mfumo wa
‘hard copy’ na kuwa katika mfumo wa sauti na picha au ‘soft copy’,”
alisema Profesa Bhalalusesa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome
akifuatilia kwa makini risala Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa (hayupo pichani).
Alisema
hadi kufikia wakati huu serikali imeshapiga hatua kubwa katika matumizi
ya Tehama ambayo katika majaribio yake yameonesha kufanikiwa na wadau
mbalimbali wa elimu wameyapongeza na kuyaunga mkono.
Profesa
Bhalalusesa alisema kwa sasa wagunduzi mbalimbali wa mifumo ya Kompyuta
inayoweza kutumika kufundishia ndio watakoonesha kazi zao na kutoa
ufafanuzi wa kina kwa majaji wataochagua kazi chache na kuzifanyia
majaribio kabla ya kuanza kutumika kufundishia.
Kwa
Upande wake Mratibu wa Mpango wa Kukuza stadi za Kusoma, Kuandika na
Kuhesabu kutoka Wizara ya Elimu, Agripina Habichi alisema mpango huo wa
matumizi ya Tehama utasaidia wanafunzi kufahamu kusoma na kuandika kabla
ya kuendelea na masomo ya darasa la tatu.
“Maonesho
haya yanafanyika katika wakati muafaka ukizingatia tunataka kupiga
hatua kubwa katika kuboresha elimu yetu. Washiriki wa maonesho haya
wamekuja kutuonesha utawaalamu wao unaoweza kutumika kufundishia.
Lengo
letu ni kuwafikia wanafunzi wengi zaidi ambapo tumeazimia kuzifikia
shule zaidi ya 2000 katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 na hivyo tutakuwa
katika kiwango bora zaidi cha utoaji wa elimu inayojitosheleza,”
alisema Habichi.
Katika
maonesho hayo serikali imesema inatarajia kuanza kutumia rasmi
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika kufundishia
wanafunzi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya elimu ambayo ni chekechea.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome
alisema matumizi ya Tehama katika ufundishaji wa wanafunzi wa chekechea
yataimarisha kiwango cha elimu.
“Dunia
imebadilika sana hasa katika sekta ya elimu na mawasiliano, hatuna budi
kuendana nayo kwa kasi ileile ya ukuaji wake kwa kuimarisha mifumo yetu
ya ufundishaji,” alisema Profesa Mchome.
Alisema
wizara yake imeanzisha mpango maalum utakaosaidia wanafunzi kujifunza
kwa njia ya kisasa ya kutumia mbinu za kielektroniki katika kujifunza na
hivyo kuimarisha uelewa na kuongeza hamasa ya ufundishaji kwa
wanafunzi.
Profesa
Mchome alisema maonesho hayo yana lengo la kupata wadau mbalimbali
waliobuni programu zinazoweza kutumika katika kufundishia kwa kutumia
mifumo ya kielektroniki na hivyo watachaguliwa wachache wenye sifa na
watakowezesha mafunzo hayo katika shule za Msingi na baadae katika ngazi
ya sekondari.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akijianda kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Sasa yamezinduliwa rasmi.
Ofisa Miradi ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akitoa maelezo ya shughuli
mbalimbali zinazofanywa na shirika lake katika kuendeleza sekta ya elimu
nchini kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa
Sifuni Mchome (kushoto) mara baada ya kuzindua maonesho hayo ambapo pia
UNESCO inashiriki. Katikati ni Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa.
Ofisa
anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari
(katikati) akimsikiliza mmoja wa wadau wa elimu aliyetembelea banda la
UNESCO kwenye maonesho ya TEHAMA yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano
wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Ofisa Miradi ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo.
Ofisa
anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari
(kulia) akiwa na wadau wengine wa elimu wakipitia makbrasha mbalimbali
katika mkutano huo.
Pichani juu na chini ni baadhi wadau wa elimu waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho hayo.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi jijini Dar walioshiriki hafla hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shule Direct, Faraja Nyalandu akipozi na wadau kwenye ukumbi wa
mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
yanakoendelea maonesho ya TEHAMA.