Marehemu Mzee Anyosisye Mwakyusa enzi za uhai wake.
Waombolezaji wakiwa wamebeba
jeneza lenye mwili wa Anyosisye Mwakyusa, baba mzazi wa mwandishi
mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Peter Ambilikile, wakati wa ibada ya
kumuombea iliyofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
Ubungo Kibangu Dar es Salaam jana, kabla ya kuusafirisha kwenda mkoani
Mbeya kwa mazishi yatakayofanyika leo.…
Marehemu Mzee Anyosisye Mwakyusa enzi za uhai wake.
Waombolezaji wakiwa wamebeba
jeneza lenye mwili wa Anyosisye Mwakyusa, baba mzazi wa mwandishi
mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Peter Ambilikile, wakati wa ibada ya
kumuombea iliyofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
Ubungo Kibangu Dar es Salaam jana, kabla ya kuusafirisha kwenda mkoani
Mbeya kwa mazishi yatakayofanyika leo.
Ndugu jamaa na marafiki wakiaga mwili wa marehemu.
Waombolezaji wakiwa kwenye ibada ya kuuga mwili wa mzee wetu Anyosisye Mwakyusa.
Familia ya marehemu ikiwa na huzuni wakati wa ibada hiyo.
Waomblezaji wakiwa ibadani.
Wafiwa wakipewa pole.
Mwanahabari Peter Ambilikile aliyefiwa na baba yake akiwa katika huzuni.
Mchungaji wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ubungo Kibangu, Kishe
Mhando (katikati), akiomba kabla ya kuanza kwa safari ya kwenda mkoani
Mbeya.
Mwili ukiondolewa kanisani.
Waombolezaji wakisubiri gari lililobeba mwili huo kuondoka kwendaa mkoani Mbeya kwa mazishi.
Ni huzuni tupu.
MZEE Anyosisye Mwakyusa ambaye ni baba wa Mwandishi Mwandamizi wa
Gazeti la Jambo Leo, Peter Ambilikile mwili wake umeagwa jana kwenda
mkoani Mbeya kwa maziko.
Anyosisye alifariki juzi jijini Dar es Salaam kutokana na ugonjwa wa saratani uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.
Ibada ya kuaga mwili wa marehemu huyo ilifanyika katika Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ubungo Kibangu jijini
Dar es Salaam jana ikiongozwa na Mchungaji Kishe Mhando wa ushirika
huo.
Mchungaji Mhando alimwelezea Mwakyusa kama mtu jasiri ambaye siku
zote alikuwa mtu wa ibada na alikuwa akihudhuria ibada zote. Aliwaambia
waumini kuwa mshahara wa dhambi ni mauti na mshahara wa kuwa na ibada ni
maisha ya milele na Bwana Mungu.
Alisema watu huwa wana ratiba yao na hakuna mtu hata mmoja anayejua
ratiba ya Mungu. "Msiba hauchagui mtoto mchanga, mtu mzima, mwanamke au
mwanaume. Mipango yote ni ya Mwenyezi Mungu, yeye ndiye anajua
anayefuata ni nani," alisema.
Mazishi ya Mzee Mwakyusa yanatarajiwa kutafanyika mkoani nyumbani
kwa marehemu eneo la Makungulu jijini Mbeya leo. Mwakyusa alizaliwa Mei
10, 1942. Alifunga ndoa yake mwaka 1968. Alifanya kazi serikalini na
alistaafu mwaka 1980.
Mwaka 1999 Mwakyusa alianza kulalamika kuwa na matatizo ya koo na
kuanza kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali, ikiwemo Hospitali
ya Ocean Road hadi kifo chake.
No comments:
Post a Comment