Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa
akizungumza na akinamama wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi,
UWT (hawapo pichani)
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akicheza wimbo wa hamasa wa kampeni
za CCM kabla ya kuanza kumnadi Dk. Magufuli kwa wanaUWT, Mkoa wa Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa
akizungumza na akinamama wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi,
UWT (hawapo pichani)
...Na wapigwe tu maana hamna namna
nyingine..' Mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mama Tunu Pinda akizungumza
na akinamama wa UWT Mkoa wa Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa Chama…
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akizungumza
na akinamama wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi, UWT (hawapo
pichani)
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akicheza wimbo wa hamasa wa kampeni
za CCM kabla ya kuanza kumnadi Dk. Magufuli kwa wanaUWT, Mkoa wa Dodoma.Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akizungumza
na akinamama wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi, UWT (hawapo
pichani)
...Na wapigwe tu maana hamna namna
nyingine..' Mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mama Tunu Pinda akizungumza
na akinamama wa UWT Mkoa wa Dodoma.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam
Kimbisa ameweka kando msimamo aliyokuwa nao awali na kuanza kumnadi kwa
nguvu mgombea wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli
huku akiahidi atafanya hivyo nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda na
shuka hadi shuka.
Kimbisa alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma alipokuwa kwenye
mkutano na akinamama wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT)
walipokuwa wakizungumza na mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM,
Bi. Samia Suluhu katika ukumbi wa NEC Makao Makuu ya Chama hicho mjini
Dodoma.
Tukio la Kimbisa kumnadi mgombea urais wa CCM, Dk. John Pombe
Magufuli pamoja na mgombea mwenza Bi. Suluhu linaonesha tayari kimbisa
amefunga ukurasa wa kutokubaliana ambao aliuonesha mapema mjini hapo
wakati wa mchakato wa chama hicho kutafuta mgombea mmoja wa urais
atakaye peperusha bendera ya CCM.
Awali mara baada ya Magufuli kuchaguliwa kupeperusha bendera ya
CCM, Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Dodoma, Kimbisa pamoja na wajumbe
wenzake wawili, yaani Sophia Simba na Dk. Emmanuel Nchimbi walizungumza
na vyombo vya habari mjini Dodoma huku wakionesha kupinga uteuzi huo
huku wakidai haukwenda sawia jambo ambalo ni tofauti na sasa.
Akizungumza katika mkutano huo aliwataka akinamama wa UWT kuhakikisha
wanashirikiana kuhamasisha kampeni za CCM na kutembea nyumba hadi nyumba
mtu kwa mtu ili kuinadi ilaya ya Chama Cha Mapinduzi na hatimaye
ushindi upatikane.
Hata hivyo tayari Dk. Nchimbi naye ameungana na kuanza kumnadi
mgombea huyo wa CCM ikiwa ni ishara ya kuvunja makundi. Mapema
akizungumza katika mkutano huo, mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mama
Tunu Pinda alisema yeye pamoja na mumewe hawawezi kuihama CCM kwa kuwa
ndiyo chama pekee chenye sera za kueleweka na zinazotekelezeka
ukilinganisha na vyama vingine.
Aliwashauri wanachama waliogombea na kushindwa kutokata tamaa na
kujaribu kukihama chama hicho kwani asiyekubali kushindwa si mshindani.
"...Napendekeza wanao hama vyama wapigwe tu, maana hamna namna nyingine
na wapigwe tu, lakini naomba tuwapige kwa kuwanyima kura huko
wanapokwenda lakini si vinginevyo," alisema Mama Tunu Pinda alipokuwa
akiwasalimu wanachama wa UWT.
Katika mkutano huo mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alitaja
vipaumbele kwa akinamama endapo watafanikiwa kuunda Serikali, ikiwemo
vile vya afya bora kwa mama na mtoto, ujasiliamali kuinua uchumi wa
akinamama katika vikundi, uwezeshaji kipembejeo na zana za kisasa kwa
akinamama wakulima, na hivyo kuwaomba wanaUWT kumchagua ili aweze
kutimiza ndoto za ahadi zake. *Imeandaliwa na www.thehabari.com .
No comments:
Post a Comment