Mgombea
ubunge wa Jimbo la Temeke kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abbas
Mtemvu (kulia), akipongezana na mgombea udiwani wa Kata ya Keko, Francis
Mtawa baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa kampeni viwanja vya
Mabembeani Keko jijini Dar es Salaam jana jioni
Mgombea
ubunge wa Jimbo la Temeke kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abbas
Mtemvu, akihutubia katika mkutano huo wa kampeni. Kulia ni mgombea
udiwani wa Kata ya Keko, Francis Mtawa.
Katibu Mwenezi wa Jimbo la Temeke, Ali Kamtande akienda jukwaani kuhutubia.
Wananchi na makada wa CCM wa eneo hilo wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Temeke,
Oliva Mwambope (katikati), akielekea jukwaani kuzungumza na wananchi
katika mkutano huo.
Mtemvu akielekea jukwaani kuhutubia.
Mgombea udiwani, Francis Mtawa akihutubia.
Wanawake
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakicheza katika mkutano wa kampeni za
ubunge na udiwani uliohutubiwa na Mgombea ubunge wa jimbo la Temeke,
Abbas Mtemvu katika viwanja vya Mabembeani Keko jijini Dar es Salaam
jana.
Hapa mgombea Udiwani Francis Mtawa (kulia), akisalimiana na makada wa CCM katika mkutano huo.
Hapa ni picha baada ya mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
MGOMBEA
ubunge wa Jimbo la Temeke kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abbas
Mtemvu amesema amejipanga vizuri kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kwa
miaka mitano mingine iwapo atachaguliwa kushika nafasi hiyo.
Mtemvu alitoa kauli hiyo wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Mabembeani Keko jijini Dar es Salaam juzi.
"Serikali
na chama chetu cha CCM tuna mipango ya maendeleo ya miaka mitano
tuliyoindaa tunaomba mtuchague tuweze kuikamalisha" alisema Mtemvu.
Alisema
wakazi wa eneo hilo wasiwe na wasiwasi wowote wala kuyumbishwa kwani
kunafedha sh. bilioni 120 kutoka benki ya dunia kupitia mradi wa UNDP
ambazo zitagaiwa katika kila Kata wilayani Temeke kwa ajili ya shughuli
za maendeleo na uboreshaji wa miundombinu na makazi ambapo kwa Keko mgao
wao ni sh.bilioni 14.
Mtemvu
alisema hivi sasa wamejiandaa kujenga barabara za kiwango cha lami
katika mitaa kadhaa ya Keko ambazo zitawekwa taa za sola.
Aliongeza
kuwa kwa kipindi ambacho walikuwa katika uongozi wamefanikiwa kujenga
miundombinu ya barabara, kuweka taa na kujenga shule za sekondary mbili
kati ya hizo zikiwa na kidato cha tano na sita pamoja na kuhimarisha kwa
huduma za afya kwa kujenga zahanati jambo ambalo ni la kujivunia.
Mtemvu
aliwaomba wananchi hao na makada wa CCM katika nafasi ya urais wampe
kura Dk. John Magufuli, Ubiunge wampe yeye na udiwani wampe Francis
Mtawa ili mambo yaende sawa.
Mgombea
udiwani wa eneo hilo Francis Mtawa aliwaomba wananchi wa eneo hilo
kutouza nyumba zao mapema bali wasubiri kukamilika kwa barabara hizo
zitakazojengwa kwa kiwango cha lami kwani zitaongeza thamani ya nyumba
hizo.
Mwenyekiti
wa CCM wa Kata hiyo, Hassan Kitigi alisema changamoto kubwa waliyonayo
wakazi wa eneo hilo ni eneo la wazi wanalofanyia mikutano kujaa maji
wakati wa mvua hivyo vijana kushindwa kuwa na sehemu ya kufanyia
shughuli zao mbalimbali pamoja na michezo.
Alitaja changamoto nyingine kuwa ni miundombinu ya barabara na kujaa maji wakati wa mvua.