FASTJET YAONGEZA SAFARI ZAKE KWENDA JOHANNESBURG SASA NI KILA SIKU - LEKULE

Breaking

29 Sept 2015

FASTJET YAONGEZA SAFARI ZAKE KWENDA JOHANNESBURG SASA NI KILA SIKU


 Mkuu wa Biashara wa Fastjet Lan Petrie (kulia), akizungumza katika semina hiyo.
 Meneja Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (kulia), akizungumza katika semina ya siku moja ya waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, iliyohusu kuongezeka kwa safari za ndege za shirika hilo kila siku kwenda Johannesburg nchini Afrika Kusini.
 Ofisa Mtendaji wa Masula ya Biashara wa Fastjet, David Chacha, akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari katika semina hiyo.
 Ofisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro akizungumza kwenye semina hiyo.(P.T)
Hapa semina ikiendelea.

Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya wateja Fastjet, Kampuni ya ndege ya Kiafrika yenye gharama nafuu  imeongeza safari zake za kimataifa kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam kwenda Johanessburg Afrika Kusini.
Safari hizo ambazo hivi sasa zitafanyika kila siku zimepangwa kwa kuwapa abiria fursa zaidi  na njia mwafaka na mbadala kwa nauli wanayoimudu.
 Utaratibu huo mpya wa safari za Johannesburg utaanza kufanya Oktoba Mosi, 2015  na tiketi kwa ajili ya safari tayari zimeshaanza kuuzwa, ambapo nauli hizo zinaanzia  kiwango cha chini cha dola za Marekani 50 kwa safari ya njia moja, bila kujumuisha  gharama za uwanja na tozo za serikali.
Akitangaza safari hizo mpya Meneja Mkuu wa Fastjet Kanda ya Afrika Mashariki tawi la Tanzania Jimmy Kibati alisema kwamba kuongezeka kwa safari  kupo sambamba na sera za kampuni hiyo za mwitiko kwa mahitaji ya wateja.
“Kila mara tunaahidi kuongeza kuongeza masafa kwenye safari zetu na hasa wateja wanapozihitaji,” alisema Kibati akibainisha kwamba kuongezeka kwa  masafa kumesisitizia  jukumu la Fastjet Tanzania kukua kwenye mtandao wake kikanda, kuufanya usafiri wa anga kuwa rahisi, salama pia waumudu.
Kibati aliongeza kusema kuwa  kuongezeka kwa utaratibu  huo  pia kumetoa uwezekano  wa kuingiza ndege  ya ziada  kwenye usafiri wa Tanzania  baadaye mwezi huu  na hivyo  kufanya idadi ya ndege A319 kufikia nne.
“Ukweli tunafurahi kwa mapokeo haya chanya ambayo Fastjet  imeshayapata ndani ya Tanzania na kwa nchi jirani ambako inafanya safari zake,” alisema Kibati.
 “Kwa kutumia gharama nafuu, Fastjet zinaifanya usafiri wa anga  kufikiw akwa urahisi kuliko ilivyokuwa awali, ambapo abiria wetu wengi wanakuwa wasafairi wa kwanza  ambao kama sio hivyo wasingeweza kusafiri kwa njia ya anga,” alisema Kibati.
Utaratibu huu mpya unafuatia  kutangazwa hivi karibuni uendeshaji ambapo ilitangaza  kuwa na idadei kubwa ya abiria kwa mwenzi. 
Katika kipindi cha Julai, Fastjet ilisafirisha  jumla ya abiria  71,763 ikiwa ni ongezeko la asilimia 36 ikilinganishwa na kipindi cha Julai mwaka jana. Jumla ya mzigo uliosafirishwa kwa mwezi Julai   ulikuwa ni sawa na asilimia 72 na kiwango cha kuwahi kilikuwa cha juu kwa asilimia 95 ya kuwasili kwa muda unaotakiwa.
Njia ya Johanessburg  ambayo inajumuisha Harare, Zimbabwe na Lusaka Zambai hivi sasa  zitawapa wateja wake  njia mbadala ya ziada kwa kusafiri kwa urahisi kwenda na kurudi kwenye maeneo yao.
Fastjet pia imeongeza mara mbili masafa yake kwenye njia mpya iliyozsinduliwa hivi karibuni  ya Dar es Salaam - Lilongwe kutoka safari mbili hadi nne kwa wiki, ambayo imefuatiwa  sio muda mrefu tangu kuanza kwa safari zake kati ya miji hiyo miwili  Julai 29, 2015. Njia ya Dar es Salaam na  Kilimanjaro kwenda Entebbe zinabakia kuwa ni safari tatu kwa wiki.
Tiketi  unaweza kufanywa kwa njia ya mtandao  kupitia tovuti ya www.fastjet.com, kupitia ofisi za fastjet kwa saa 24   au kupiga simu namba +255 784 108 900, na malipo yanaweza kufanyika kwa fedha taslim au kupitia kwenye mitandao ya simu ya Mpesa na Tigopesa.