Kocha
Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro, Charles Mkwasa amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo
wa kesho dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya
Afrika mwaka 2017.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo
Karume, Mkwasa amesema vijana wake wapo katika hali nzuri kuelekea
kwenye mchezo huo wa kesho ambao ni muhimu kwa Taifa Stars.
“Tumefanya
mazoezi kwa takribani siku kumi, vijana wako katika hali nzuri ya
mchezo, uwezo waanaouonyesha mazoezini ni wa hali ya juu na unatupa
matumaini ya kufanya vizuri” Alisema Mkwasa.
Aidha
Mkwasa amesema katika mpira hakuna kinachoshindakana, anatambua Nigeria
ni timu kubwa Afrika, wameshatwaa ubingwa wa Afrika mara tatu, lakini
mpira wa sasa lolote linaweza kutokea, hivyo sisi tumejiandaa vilivyo
kufanya vizuri katika mchezo huo.
Mwisho
Mkwasa amesema wamejindaa vizuri kwa mchezo huo wa kesho, na kuwaomba
watanzania kuja kuwapa sapoti wachezaji uwanjani kwa kuwashangilia muda
wote wa mchezo, na kusema kikosi chake hakina mchezaji majeruhi hata
mmoja kuelekea kwa mechi hiyo.
Mechi
hiyo ya kesho jumamosi itachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Rwanda
ambao ni Louis Hakizimana (mwamuzi wa kati) Honore Simba (mwamuzi
msaidizi), Jean Bosco Niyitegeka (mwamuzi msaidizi), Abdoul Karim
Twagiramukiza (mwamuzi wa akiba) na kamisaaa wa mchezo ni Charles
Kasembe kutoka nchini Uganda ambao wote tayari wameshawaili jijini Dar
es salaam tangu jana jioni.
Tiketi za
mchezo huo tayari zimeshaanza kuuzwa leo saa 4 kamili asubuhi katika
vituo vya (i) Ofisi za TFF – Karume , (iii) Mbagala – Dar live, (iv)
Ubungo – Oilcom, (v) Makumbusho – Stendi, (vi) Uwanja wa Taifa, (vii)
Mwenge – Stendi, (viii) Kivukoni- Feri, (ix) Posta – Luther House, (x)
Big Bon – Msimbazi Kariakooo
Viingilio
vya mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika
(AFCON Qaulifier 2017) kundi G itakua ni VIP A Tsh 40,000, VIP B Tsh
30,000, VIP C Tsh15,000, Rangi ya Machungwa (Orange) Tsh 10,000, na viti
vya rangi ya Bluu na Kijani Tsh 7,000.
TFF
inawaomba watanzania, wapenzi na wadau wa mpira wa miguu kununua tiketi
za mchezo huo katika magari yaliyopo kwenye vituo vilivyotajwa ili
kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi zisizokuwa halali.
Jeshi la
Polisi nchini kwa kushirikiana na idara nyingine za kiusalama wameandaa
usalama wa kutosha katika kuelekea kwenye mchezo na kuhakikisha kila
mpenzi wa mpira wa miguu anaingia kushuhudia mchezo huo salama na
kuondoka salama.
Mchezo
huo utaanza saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki utachezeshwa na
waamuzi kutoka nchini Rwanda ambao wanatarajiwa kuwasili leo jioni
pamoja na kamisaa wa mchezo huo.
Wakati
huo huo Kikosi cha wachezaji 23 cha timu ya Taifa ya Nigeria (Super
Eagles) kimewasili nchini jana usiku na kufikia katika hoteli ya
Kempsink iliyopo eneo la Posta ambapo leo jioni watafanya mazoezi katika
uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es salaam.
Kikosi
hicho cha Nigeria kinachoongozwa na kocha Sunday Oliseh kinawajumuisha
makipa Ikeme Onoro, Ezenwa Ikechukwu, walinzi Thomas Olufemi, Balogun
Aderemi, kwambe Solomon, Omeruo Keneth, Ekong William, Oboroakpo Austin,
Akasi Chima, na Madu Kingsley.
Wengine
ni viungo Ibrahim Rabiu, Muhamed Usman, Uzochukwu Izunna, Haruna Lukman,
Nwankwo Obiora, Igboun Emeka, washambuliaji Simon Daddy, Ujah Anthony,
Emenike Chinenye, Musa Ahmed, Aggreh Obus na Eduok Samuel.
No comments:
Post a Comment