JESHI la polisi kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani Iringa jana walitumia mabomu ya machozi kuwakamata wafuasi zaidi ya 61 wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema ) akiwemo mgombea ubunge wao jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kwa tuhuma za kumpiga mawe mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Iringa na wananchi waliokuwa wakitoka katika mkutano wa mgombea Urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dr John Magufuli.
Imeelezwa
kuwa wafuasi hao ambao wengi wao ni vijana walikuwa wamekutana
katika eneo la kambi ya kampeni ya Chadema iliyopo eneo la Hoteli
ya Sambala jirani na kambi ya kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) kwa
ajili ya kikao cha ndani toka majira ya mchana na jioni ndipo
walipofanya vurugu hizo wakati wananchi wakitoka katika mkutano wa
kampeni za mgombea huyo wa Urais wa CCM.
Kamanda
wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi amewaeleza waandishi wa
habari kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 12;30 jioni
baada ya wafuasi hao kufunga barabara kuu ya Iringa –Dodoma na
kufanya vurugu hizo kwa kuwarushia mawe wananchi waliokuwa wakitoka
katika mkutano wa kampeni za Dr Magufuli uwanja wa Samora.
Amesema
kuwa wakati jeshi la polisi likiwa katika mkutano wa mgombea huyo
wa Urais wa CCM walipokea taarifa kuwa kuna vijana wa boda boda
zaidi ya 150 walikuwa wakijikusanya kuelekea katika eneo hilo la
Sambala Lodge na baada ya kufuatilia ndipo walibaini kuwa wanakwenda
katika kikao chao cha ndani na kwa kawaida jeshi la polisi
halikatazi watu kufanya vikao vyao vya ndani .
“Jeshi
la polisi halizuii wanachama wa chama chochote cha siasa kufanya
vikao vya ndani kwani ni haki yao ya kisheria na kikatiba,lakini
baada ya kikao chao kumalizika vijana hao walitoka nje ya ukumbi
huo uliopo kando kando ya barabara na kuanza kufunga barabara na
kucheza muziki katikakati ya barabara na kuzuia watumiaji wengine wa
barabara
"Baada ya vurugu hizo nilimuagiza mkuu wa FFU kwenda kuwatoa watu hao barabarani ila walipuuza na kuishia kumpiga mawe na baadae kukimbilia kujifungia katika Lodge hiyo ya Sambala eneo ambalo wamefanya kama makao makuu ya Kampeni za Chadema “ alisema kamanda Mungi.
"Baada ya vurugu hizo nilimuagiza mkuu wa FFU kwenda kuwatoa watu hao barabarani ila walipuuza na kuishia kumpiga mawe na baadae kukimbilia kujifungia katika Lodge hiyo ya Sambala eneo ambalo wamefanya kama makao makuu ya Kampeni za Chadema “ alisema kamanda Mungi.
Amesema
wakati wa vurugu hizo baadhi ya vijana waliumia kwa kuruka ukuta
na wengine kwa kuanguka wakati wakijaribu kukwepa kukamatwa na kuwa
wale wote waliokamatwa watafikishwa mahakamani wakati wowote
kuanzia sasa na kuwa miongoni mwao yumo mgombea ubunge jimbo
hilo,Mchungaji Msigwa .
Mbali
ya mchangaji Msigwa wengine waliokamatwa kwa tuhuma za vurugu
hizo ni pamoja na mgombea udiwani kata ya Gangilonga ambae pia ni
mkuu wa kambi hiyo Dady Igogo
Hata hivyo, taarifa iliyotufikia jion hii inaarifu kuwa Mchungaji Msigwa na wafuasi hao 61 wameachiwa kwa dhamana leo.
Hata hivyo, taarifa iliyotufikia jion hii inaarifu kuwa Mchungaji Msigwa na wafuasi hao 61 wameachiwa kwa dhamana leo.