Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Saed Kubenea amefichua mbinu za Tume ya uchaguzi (NEC) kukutana na mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Ukumbi wa Kilimanjaro Hoteli.
Kubenea
amesema kuwa Maofisa wa tume hiyo walikutana na mgombea ubunge kupanga
mbinu ya kutengeneza vitambulisho feki vya kupigia kura ameahidi kutaja
jina lake wakati wa ufunguzi wa Kampeni za ubunge siku ya Jumapili.
Ameongeza
kuwa wanajua njama zinazofanywa na NEC na watakuwa wanaweka wazi kila
kitu ambacho tume hiyo katika mikutano yao ya kampeni alisema katika
kampeni zao wataelezea madhaifu ya chama tawala kwa miaka 54.
Kubenea
amesema kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM ameanza kufanya kampeni
chafu ambapo aliandaa vijana feki wa chama hicho na kuwavalisha nguo za
chadema na kuwaambia waandamane na kusema wanamuunga mkono aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilibroad Slaa.
Ameongeza
kuwa tayari amemwagiza mwanasheria wake pamoja na wachama kupeleka
malalamiko Nec ambayo wataambatanisha na Cd inayomuonyesha Mgombea huyo
akiwa anajisifia kwa kitendo alichokifanya.
Amesema
kitendo alichokifanya Masaburi ni kinyume na utaratibu wa maadili ya
uchaguzi pia ameongeza kuwa kama wao wasivyochana mabango ya vyama vya
upinzani nao wasichane ya kwao “Tutawachukulia hatua za kisheria vijana
wanaopewa Sh 10,000 na wagombea kuchana mabango yetu kwa sababu
tunaushaidi,”
Kubenea
amemtupia lawama Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Bernard Membe kwa kuwatisha waangalizi wa Uchaguzi kutoa maoni, matokeo
kabla ya NEC kutangaza matokeo na kusema mgombea wa CCM ndiye atakaye
shinda.
No comments:
Post a Comment