Kilichomlaza Lema rumande jana - LEKULE

Breaking

5 Sept 2015

Kilichomlaza Lema rumande jana


gombea ubunge jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na UKAWA, Godbless Lema na wenzake wanne wameachiliwa kwa dhamana leo baada ya kushikiliwa na polisi tangu jana.
Polisi mkoani Arusha waliwakamata watuhumiwa hao jana jioni mara baada ya kuzindua kampeni ya kuwania ubunge katika jimbo hilo katika Shule ya Msingi Ngarenaro.
Wakisomewa mashtaka katika mahakama ya Arusha, Lema amedaiwa kulizima gari lake wakati wakitokea kwenye mkutano wa kampeni, hali iliyowafanya wafuasi wake kuanza kulisukuma hivyo kusababisha maandamano pasipo kuwa na kibali cha polisi. Lema na wenzake wameyakana mashtaka dhidi yao. 

No comments: