WIZARA ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, imewataka watu waliosambaza uvumi katika mitandao ya kijamii kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, kuwa amelazwa nje ya nchi kwa ugonjwa, kuomba radhi mapema la sivyo watachukuliwa hatua.
Taarifa
iliyotolewa jana na msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa, Luteni Kanali Juma Sipe, imeweka wazi kuwa Jeshi na Wizara kwa
kushirikiana na mamlaka husika, wanachunguza watu hao na kuwataka waombe
radhi mapema kabla ya hatua hizo.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, Jenerali Mwamunyange ni mzima wa afya na
aliondoka nchini Jumanne iliyopita Septemba 22, 2015, saa 10.45 jioni
kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates kwenda Rome, Italia kwa ziara
ya kikazi kwa mwaliko wa Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo, Jenerali Claudio
Graziano.
“Tunapenda
kuwahakikishia wananchi kuwa Jenerali Mwamunyange pamoja na ujumbe wake
wanaendelea na ziara hiyo kama ilivyopangwa na amesikitishwa na uvumi
huo,” alisema Sipe.
Sipe
alisema uvumi huo ni matumizi mabaya ya uhuru wa habari na kuupotosha
umma na umeleta usumbufu kwa familia ya Jenerali Mwamunyange, Jeshi na
Taifa kwa ujumla.
Alisisitiza kuwa watu walisambaza uzushi huo kwamba Jenerali Mwamunyange amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan iliyopo Nairobi, Kenya, huku wengine wakidai kuwa yuko nchini India kwa matibabu, kumuomba radhi kwa kutambua kuteleza kwao.
Alisisitiza kuwa watu walisambaza uzushi huo kwamba Jenerali Mwamunyange amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan iliyopo Nairobi, Kenya, huku wengine wakidai kuwa yuko nchini India kwa matibabu, kumuomba radhi kwa kutambua kuteleza kwao.
“Taarifa
hizo ni uongo wenye kila dalili ya kutengenezwa kwa lengo la kuwatia
hofu Watanzania juu ya usalama wa kiongozi huyu wa juu wa majeshi yetu,
Mkuu huyo wa Majeshi ya Ulinzi, ni mzima wa afya na hayupo nchini Kenya
wala sio India kama ilivyoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo
vya habari,” alisema Sipe.
Sipe
alionya kwamba kuacha kuomba radhi, itatafsirika kuwa ni kukiri kueneza
uzushi huo kwa makusudi na kwa dhamira fulani na hivyo kushawishi hatua
zaidi kuchukuliwa. Alisema wizara hiyo imesikitishwa na tabia hiyo ya
uzushi inayopingana na weledi na kanuni za uandishi wa habari.
Jenerali Mwamunyange akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake
na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.
Jenerali Mwamunyange akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake
na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.
Jenerali Mwamunyange
akiteta jambo na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.