RAIS
Jakaya Kikwete amewatunuku nishani za utumishi uliotukuka, utumishi
mrefu na tabia njema maofisa wa majeshi mbalimbali 30. Kati ya maofisa
hao, 10 ni kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), 10
kutoka Jeshi la Polisi na 10 wengine wanatoka Jeshi la Magereza.
Akiwataja
maofisa waliopata nishani za utumishi uliotukuka, Mkurugenzi wa
Shughuli za Ikulu Julius Magore, alisema nishani hiyo hutunukiwa kwa
maofisa walio hai wa cheo cha Meja kwenda juu kwa JWTZ na kwa Polisi
hutolewa kwa Mrakibu au maofisa Waandamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa
waliotimiza si chini ya miaka 20.
Waliotunukiwa
nishani hiyo ni Meja Jenerali Yacub Mohammed, Brigedia Jenerali Jacob
Kingu, Kanali Fadhil Nondo, Luteni Kanali Ian Haule, Kamishna wa Polisi
Elice Mapunda, Naibu Kamishna wa Polisi Samson Kasala, Rashid Omar,
Mohammed Mpinga na Gaston Sanga.
Wengine
ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Gideon Nkana, Augustine Mboje
na Venant Kayombo. Aidha, Magore alisema Nishani ya Utumishi Mrefu
hutunukiwa kwa maofisa walio kwenye utumishi hai wenye Kamisheni wa JWTZ
na maofisa waliotangazwa gazetini wa Polisi, Magereza na Idara ya
Usalama wa Taifa waliotimiza utumishi wa miaka isiyopungua 15 wakiwa
wenye tabia njema ya kuweza kusifiwa.
Aliwataja
maofisa waliotunukiwa nishani hiyo kuwa ni Kanali Mary Hiki, Kanali
Msafiri Hamisi, Meja Bernard Mlunga, Kamishna wa Polisi Valentino
Mlowola, Naibu Kamishna wa Polisi Ally Lugendo, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi Mboje Kanga, ACP Vincent Marissa, Bakari Ndembo na Vincent
Karata.
Aidha,
alisema Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema hutunukiwa kwa maofisa
wasiokuwa na kamisheni walio katika utumishi wa JWTZ na wakaguzi,
wakaguzi wasaidizi, stesheni sajini, sajini na koplo wa polisi na
magereza.
“Wanaotunukiwa
nishani hii ni wale waliotumikia jeshi mfululizo kwa muda usiopungua
miaka 15 katika vyeo hivyo watumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa
waliotumikia idara hizo mfululizo kwa tabia ya kuweza kusifika,”
alisema.
Aliwataja
waliotunukiwa kuwa ni Ofisa Mteule Atilio Mgimbe, Sajini Taji Banda,
Sajini Taji Haji, Inspekta Ally Haji, Sajini Charles Simon, Staff Sajini
Asia Maji, Inspekta Msaidizi Rukia Mopey, Sajini Yasin Msangi na Sajini
Regina Elias.

No comments:
Post a Comment