Jeshi Ladhibiti Kambi Burkina Faso - LEKULE

Breaking

30 Sept 2015

Jeshi Ladhibiti Kambi Burkina Faso

Burkinafaso
Serikali ya mpito ya Burkina Faso imesema jeshi limedhibiti kambi ya vikosi vya ulinzi vya Rais vilivyofanya mapinduzi mapema mwezi huu.
Maafisa wametangaza tukio hilo kwa njia ya Televisheni, haijafahamika kama kuna madhara yeyote yalijitokeza.
Awali, Mwandishi wa BBC mjini Ouagadougou alisema milio ya risasi na milipuko ilisikika na moshi kutapakaa kutoka eneo la kambi.
Kiongozi wa mapinduzi,Jenerali Gilbert Diendere,ambaye haifahamiki alipo aliitisha kikosi chake kwa ajili ya kusalimu amri kuepuka umwagaji damu.
Aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa kuwa alikuwa na wasiwasi wa kuwepo kwa idadi kubwa ya waliopoteza maisha wakati kambi hiyo ikidhibitiwa.
Kufuatia tukio hilo, Uwanja wa Ndege mjini humo ulilazimika kufungwa huku wakazi wakiamriwa kubaki nyumbani.

Serikali imesema imesambaratisha Vikosi vya ulinzi vitiifu kwa Rais wa zamani wa nchi hyo, Blaise Compaore na Jenerali Diendere.