Insignia kusaidia jamii katika elimu - LEKULE

Breaking

16 Sept 2015

Insignia kusaidia jamii katika elimu


INSIGNIA_LOGO-page1
Kitendo cha kampuni au taasisi kuisaidia jamii kinageuka kuwa cha kisheria katika baadhi ya nchi na kwa nchi mbalimbali bado ni jambo la uamuzi. Watafiti wamegundua, kampuni tatu kati ya kila kampuni nne tayari wanaisaidia jamii au wana mpango wa kuisaidia jamii, miaka michache ijayo. Asilimia 58 ya makampuni yamethibitika kuwa na bajeti kila mwaka kwa ajili ya uendelezaji wa shughuli hizi.
Tafiti pia zimeonesha kuwa kwa kiasi kikubwa; Zaidi ya asilimia 80 ya kampuni zinachagua elimu kama eneo muhimu la shughuli zao endelevu.
Kampuni inayoongoza Tanzania kwa uzalishaji wa rangi ya Insignia Limited, inachukulia uwajibikaji kwa jamii kama sehemu muhimu ya sera ya kampuni hiyo. Insignia inatoa mchango mkubwa katika kusaidia jamii ya kitanzania kupitia kujitolea kwake katika elimu.
Kwa mujibu wa Bw. Kishan Dhebar, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Insignia Limited, moja kati ya viashiria muhimu vya maendeleo katika jamii ni elimu. Ambapo pia inachangia jamii kuweza kujitegemea na maendeleo yenye usawa. Pamoja na kuongezeka kwa uelewa wa Dunia juu ya namna gani biashara inachangia katika malengo ya jamii, Insignia Limited imetambua kuwa elimu inahitaji mchango mkubwa zaidi kutoka kwa makampuni.
“Tunaamini kabisa kwamba tunaweza kuleta mabadiliko kwa kutoa misaada kwa wahitaji na wasiojiweza na ndio maana tunatoa msaada sana katika Elimu. Anasema Bw. Kishan
Mpaka hivi sasa Insignia Limited tumeisadia jamii katika kuendeleza elimu, ikiwa ni pamoja na; kutoa msaada wa kifedha kwa  shule ya vipofu na viziwi Ilala, Kutoa kozi chuo cha VETA na vyuo vingine vya ufundi jijini Dar es Salaam, juu ya misingi ya mbinu mbalimbali  za upakaji rangi zinazohitajika kitaalamu, na pia kutoa misaada ya kifedha inayohitajika zaidi kwa shule za umma mikoa kama vile Moshi, Dodoma na Dar es Salaam. Anathibitisha Bw. Dhebar.
Ingawa inafahamika kuwa utoaji wa elimu ni wajibuwa serikali, makampuni na viwanda vinatoa maendeleo endelevu ya taaluma, mafunzo na misaada mbalimbali katika sekta ya elimu.
Mara nyingi, makampuni na jamii kwa ujumla wamekuwa wakikabiliana na changamoto, kama vile ujuzi usioendana na mahitaji, ambapo wanaohitaji ajira hawana ujuzi fulani. Kuondoa changamoto hii Insignia Limited pia imewekeza katika mipango ya mafunzo ambayo yanaimarisha ujuzi wa wapaka rangi wa hapa nchini Tanzania. Kampuni hiyo imezingatia kiwango cha ushindani miongoni mwa mafundi rangi na tangu mwaka 2003 ili kuongeza ufahamu wa kazi yao kwa kiwango kipya. Zaidi ya wapaka rangi 100,000 Tanzania wamepata fursa ya mafunzo pasipo gharama yoyote kutoka Insignia Limited.
Wapaka rangi walipata maarifa na ujuzi wa hali ya juu kuhusu rangi kama vile rangi ni nini, faida, viungo, kuchanganya rangi, aina mbalimbali za kuta sifa zao na mbinu za upakaji. Mafunzo pia yamekuwa jukwaa la kushughulikia malalamiko kuanzishwa kwa bidhaa mpya, mbinu na hatua za usalama.
Mafunzo haya pia yana thamani kifedha kwa wapaka rangi ambapo wanafundishwa mbinu za kuwawezesha kuwa na ufahamu zaidi wa njia bora za kudhibiti gharama ikiwa ni pamoja na kupunguza makosa wakati wa kazi kwa ajili ya kufikia matokeo. Utoaji wa vyeti vya ushiriki mwishoni mwa mafunzo kutoka kwa kampuni inayotambuliwa kumewanufaisha watu wengi zaidi katika kupata ajira.
Mr Kishan anasisitiza kuwa wanaona fahari sana kwa juhudi zao katika shughuli za kujitolea kuisaidia jamii kama kampuni inayoongoza Tanzania kwa uzalishaji wa rangi. Pia alieleza juu ya mkakati wao endelevu juu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira. Tunajitoa kwa upande wa elimu na mazingira kitu ambacho binafsi tunakiona kama jambo jema kwa maaendeleo ya biashara kwa ujumla. Anasema Mkurugenzi.
Uwajibikaji kwa jamii unaleta fursa kwa makampuni na serikali. Kupitia kujtolea kwa jamii kampuni na taasisi mbalimbali hutoa mchango wenye manufaa kwa biashara na jamii kwa ujumla.

No comments: