MGOMBEA
urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna
Mghwira, amesema akichaguliwa kuwa rais kwenye Uchaguzi Mkuu ujao,
atamaliza migogoro ya ardhi kati ya wakulimana wafugaji inayoendelea
katika mikoa mbalimbali.
Mghwira
aliyasema hayo jana katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye
Uwanja wa Toboa Tobo, Wilayani Malinyi, mkoani Morogorona kuongeza kuwa,
migogoro mingi ya ardhi inayohusisha makundihayo inachangiwa na uongozi
mbovu.
Alisema
uongozi wa CCM umeshindwa kusimamia matumizi bora ya ardhi au kutoa
upendeleo kwa kundi moja, hivyo akiwa rais, atahakikisha migogoro hiyo
inaisha katika muda mfupi na kuweka viongozi makini ambao hawawezi
kupokea rushwa ili kupendelea upande mmoja.
"Baadhi
ya wananchi wanashindwa kutumia kilimo ili waondokane na umaskini
kutokana na baadhi ya watendaji kutumia migogoro ya ardhikwa lengo la
kujinufaisha, hivyo wapigieni kura wagombea wa ACT tuweze kuitatua
changamoto hii na kuwaletea maendeleo.
"Vipaumbele
vyetu viko vinne ambavyo ni elimu, hifadhi ya jamii, afya na uchumi
shirikishi ambavyo ni muhimu kwa maisha ya Watanzania wakiwemo wakulima,
wafugaji, wafanyabiashara, pia tutaanzisha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
ili wapate mikopo," alisema.
Naye
mgombea mwenza, Hamad Musa Yusuph, alisema huu ni mwaka wa mageuzi na
ili kuleta maendeleo ya kweli lazima wakazi wa Malinyi wamchague
mgombea ubunge wa ACT-Wazalendo kwa kuwa CCM haiwezi kuleta maendeleo
kwa miaka mitano ijayo.
Mgombea
ubunge wa jimbo hilo, Idaya Usangu, alisema kuna matatizomengi jimboni
humo ikiwemo migogoro ya ardhi, ubovu wa barabara unaosababisha wananchi
kushindwa kusafiri hasa wakati wa masika kitu ambacho akichaguliwa
atakipatia ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment