IMG_6739
Meneja Miradi na Biashara wa DSE, Patrick Mususa.
Na Ally Daud – MAELEZO, Dar Es Salaam
IDADI ya mauzo katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE) imeshuka  kwa asilimia 78 kutoka Tsh. Bilioni 29.8 hadi Tsh. Bilioni 6.4 kwa kipindi cha wiki moja iliyopita.
Aidha idadi ya hisa zilizouzwa katika soko  hilo pia zimeshuka kwa asilimia 60 kutoka Tsh. Milioni11.2 hadi kufikia Tsh. Milioni 4.3 kutokana na makampuni mengi kutowekeza katika soko la hisa.
Akizungumza na waaandishi wa habari leo (Jumatatu Septemba 07, 2015) Meneja Miradi na Biashara wa DSE, Patrick Mususa alisema kuwa hata hivyo idadi ya mtaji katika soko umekuwa kutoka tilioni 21.8 hadi tilioni 21.9 ikiwa ni pamoja na ongezeko la idadi ya mtaji wa makampuni ya ndani  kutoka Tsh. Trilioni 9.7 hadi Tsh. Trilioni 9.9.
Aidha Bw.Mususa ameitaja benki ya CRDB kuwa ndiyo inayoongoza kuuza hisa zake katika soko hilo ikiwa na asilimia 91, ikifuatiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ikiwa na asilimia 7 na Benki ya NMB ikiwa na asilimia 0.5.
Kwa mujibu wa Mususa alisema kampuni ambazo zinaongoza kwa ongezeko la bei katika soko la hisa kuwa ni Uchumi Super Market ikiwa na asilimia 5.5 ikifuatiwa na Benki ya KCB ikiwa na asilimia 4.4 pamoja na benki ya NMB 3.5
“Viashiria vya soko katika huduma za kibenki vimeongezeka kwa alama 62, hisa za benki ya NMB  zimeongezeka kwa pointi 3.5 ikifuatiwa na sekta ya viwanda kwa alama 20  kutokana na ongezeko la bei ya hisa za TBL”
Mususa alifafanua kuwa pamoja na viashiria vya kibiashara kushuka kwa alama 4 kulikochangiwa na punguzo la bei ya hisa za swissport kwa asilimia 0.13, kwa ujumla kiashilia cha soko kimeongezeka.
“DSE tumeboresha huduma zetu kwa kuanzisha huduma ya kimtandao ya  DSE mobile Trading  ili kuwawezesha watumiaji wa huduma hizo kujiunga , kununua na kuuza hisa kupitia simu ya mkononi kwa kupiga  *150*36#”.