Habre azua kihoja mahakamani - LEKULE

Breaking

8 Sept 2015

Habre azua kihoja mahakamani



Habre amekataa kuitambua mahakama hiyo
Kesi ya uhalifu wa kivita dhidi ya kiongozi wa zamani wa Chad Hissene Habre inaendelea hii leo katika mji mkuu wa Senegal Dakar licha ya kiongozi huyo kukataa kuitambua mahakama hiyo.
Bwana Habre alilazimishwa kuingizwa mahakamani kwa nguvu alipokataa kuingia mwenyewe.
Kiongozi huyo alishikwa na walinzi alipomfokea hakimu pale upande wa mashtaka ulipoanza kusoma orodha ya majina ya watu waliouawa ama kupotea wakati wa utawala wake.
Bwana Habre anatuhumiwa kwa kuamrisha mauaji ya watu 40,000 wakati wa utawala wake mnamo miaka ya 80.

Habre alilazimishwa kuingizwa mahakamani kwa nguvu
Pia anakabiliwa na mashtaka ya mateso na uhalifu dhidi ya ubinadamu.  BBC
Kesi hiyo ilihairishwa mwezi Julai baada ya bwana Habre kupinga mahakama hiyo akiitaja kuwa isiyo halali ambapo pia aliwashauri mawakili wake wasihudhurie.
Mahakama baadaye ilimpa mawakili ambao waliomba takriban siku 45 iliwajifahamishe yanayojiri katika kesi hiyo.
Siku 45 baadaye mawakili watatu walioteuliwa wamepata muda wa kutosha kuiangalia kesi hiyo lakini mteja wao hawatambui na amekataa kuwasiliana nao.
Jaji wa mahakama ya Burkinabe, Gberdao Gustave Kam ataamua iwapo kesi hiyo itaendelea bila upande wa utetezi wa Hissene Habre.
Tangu mwanzo wa utaratibu wa kesi hiyo, Hissene Habre, mwenye umri wa miaka 72, amekuwa akikataa kutambua uhalali wa mahakama maalum ya Afrika, ambayo iliundwa na Umoja wa Afrika mwaka 2013, ili kushugulikia kesi yake nchini Senegal.
Rais huyo wa zamani wa Chad hajawahi kujibu maswali ya jaji.

Habre anatuhumiwa kwa kuamrisha mauaji ya watu 40,000
Afisa wa Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, Reed Brody amesema kwa kukataa kushirikiana na mahakama, Habre anajaribu kuchelewesha utaratibu wa mahakama, ambayo ina bajeti ya dola milioni 9.5.
Kucheleweshwa kwa kesi hiyo kwa siku 45 kutaongeza bajeti kwa asilimia tisini.
Kesi hiyo ilikadiriwa kuchukua muda wa siku 90 pekee.
Waathirika ambao walifanya kampeni ya miaka 25 kuhakikisha ameshtakiwa wanatarajia kuwa mahakama hiyo itatenda haki.

Rais huyo wa zamani wa Chad hajawahi kujibu maswali ya jaji
Hii ni mara ya kwanza rais wa nchi kushtakiwa katika nchi nyingine ya Afrika kwa shutma za unyanyasaji, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.
Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo maalum atajaribu kuwasilisha ushahidi kuonyesha kuwa Habre aliamuru mauaji na unyanyasaji wa maelfu ya watu waliompinga kisiasa.
Tume ya ukweli iliyoundwa kuchunguza madai hayo ilipata ushahidi wa mauaji ya takriban watu 4,000 na ikakadiria kuwa huenda idadi hiyo ikawa mara 10 zaidi.

No comments: