Dar es Salaam.
Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema anasubiri kwa hamu kujibiwa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kama alivyotangaza kanisani kwake Jumapili iliyopita.
Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema anasubiri kwa hamu kujibiwa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kama alivyotangaza kanisani kwake Jumapili iliyopita.
Akiwa
kanisani hapo juzi, Askofu Gwajima alikaririwa akisema atajibu mapigo
kuhusu tuhuma zilizotolewa dhidi yake na Dk Slaa katika hotuba yake ya
Septemba Mosi.
Katika hotuba hiyo, Dk Slaa alimwita kiongozi huyo wa Kiroho kuwa ni mshenga wa Edward Lowassa kwa Chadema.
Mwanasiasa
huyo mstaafu alizungumza kwenye Hoteli ya Serena baada ya kutoelewana
na viongozi wenzake wa Chadema kumpokea Lowassa ajiunge na chama hicho.
“Ukweli
unasemwa kama ulivyo, hauyumbishwi yumbishwi, kama anataka kukanusha au
kujibu chochote basi afanye hivyo,” alisema Dk Slaa.
Alisema anamshangaa Askofu Gwajima alipohojiwa na gazeti
hili baada ya hotuba yake alikanusha kuwa mshenga hali akijua kuwa
alizungumza naye (Dk Slaa) wakiwa pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Chadema,
Tundu Lissu, mke wake, Josephine Mushumbusi na baadhi ya viongozi wa
chama hicho.
“Ninachosema kama hana hofu ya Mungu aendelee na akitaka kukanusha au kujibu mapigo ajibu,” alisema.
Hata
hivyo, Dk Slaa alikanusha kuwatuhumu maaskofu 30 kati ya 34 kupewa
fedha na badala yake alisema alikuwa ananukuu kile alichosema Gwajima
katika kikao kilichofanyika Julai 27.
“Askofu Gwajima alisema hayo wakati akinishawishi nimkubali Lowassa nikiwa nyumbani kwangu Julai 28,” alisema Dk Slaa.
Pia,
alikanusha kumtuhumu Rostam Aziz kutoa kiasi cha Sh15 bilioni kwa ajili
ya kampeni badala yake alisema maneno hayo yalitamkwa na Askofu Gwajima
mwenyewe.
No comments:
Post a Comment