Na RFI
Nchi 28
wanachama wa Umoja wa Ulaya zimepitisha Jumanne wiki hii kwa "idadi
kubwa" mgawanyo wa wakimbizi 120,000 barani Ulaya, na kupingwa na nchi
nne za Mashariki kwa idadi iliyopendekezwa na Brussels.
" Uamuzi
juu ya kuhamishwa kwa watu 120,000 umepitishwa na idadi kubwa ya nchi
wanachama", imepongeza kwenye Twitter Ofisi ya Rais wa Luxemburg, ambaye
ni mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya.
Tume ya Ulaya, kupitia pendekezo hilo, ambayo imezigawa nchi za Ulaya imepongeza "uamuzi huo muhimu. "
Uamuzi
huo umechukuliwa na idadi kubwa ya nchi zilyoshiriki kikao hicho na
kupingwa na Jamhuri ya Czech, Hungary, Romania na Slovakia ambazo
zimepiga kura ya kupinga. Mjumbe wa Finland hakutoa msimamo wake.
Poland, ambayo mpaka sasa ilikuwa moja ya nchi za kambi ya upinzani,
imejiunga na kambi ya walio wengi.
" Hivi
karibuni, tutagundua kwamba mfalme hana uamzi. Utaratibu mzuri umepotea
leo", waziri wa mambo ya ndani wa Jamhuri ya Czech, Milan Chovanec,
amelaumu kwenye Twitter.
" Baadhi
watasema kwamba Ulaya imegawanyika kwa sababu hatukufikia uamzi kwa
makubaliano lakini tuko katika hali ya dharura ", amesema waziri wa
Uhamiaji wa Luxemburg, Jean Asselborn, mkandarasi mkuu mazungumzo.
" Ilikuwa ni lazima leo kupitisha nakala hii ya kisheria, bila hivyo Ulaya ingegawanyika zaidi ", Jean Asselbom amebainisha.
" Ulaya
imechukua majukumu yake kwa wakimbizi ", amesema Rais wa Ufaransa
Francois Hollande, ambaye yuko ziarani mjini London, nchini Uingereza.
Hatua ya
dharura iliyopendekezwa na Tume ya Ulaya inahusu wakimbizi 120,000
kutoka Syria, Iraq na Eritrea waliowasili tangu mwishoni mwa mwezi
Agosti nchini Ugiriki na Italia, nchi ambazo ziko kwenye mstari wa mbele
kwa kukabiliwa na mgogoro wa uhamiaji katika bara la kale tangu mwaka
1945.