Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr.
John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji wa Meatu mkoani Simiyu
wakati alipofanya mikutano mbalimbali katika wilaya za Busega, Meatu,
Bariadi na Itilima akiwaomba wananchi wa wilaya hizo kumpigia kura za
ndiyo ili kuwa rais wa Tanzania na kuwatumikia watanzania katika nafasi
hiyo kubwa.
Amewaambia
wananchi hao kwamba ametekeleza miradi mbalimbali ya barabara nchini
kwa mafanikio akiwa Waziri wa Ujenzi na alikuwa akitumwa, Lakini sasa
atakuwa akiwatuma yeye watendaji na kuwasimamia. Jukumu ambalo yeye
binafsi anaweza kulitekeleza kwa mafanikio makubwa, uaminifu, uchapakazi
na ukweli ili kuleta maendeleo na mabadiliko ya kweli kwa watanzania wa
kipato cha chini lakini pia kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.
Ameongeza
kwamba anataka Tanzania iwe nchi ya viwanda ili kukuza ajira kwa vijana
waliowengi na kukuza uchumi wa taifa kuptia sekta hiyo ya viwanda
ambapo ameelezea kwamba serikali yake itajenga viwanda Vodogo, Vya kati
na Vikubwa ambayo vinaweza kutengeneza bidhaa mbalimbali kama mikoba,
mikanda, viatu, Nguo na bidhaa nyingine nyingi.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr.
John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia mkutano wake wa
kampeni mjini Meatu mkoani Simiyu leo.
Umati wa wananchi wakiwa wamefurika kwenye mkutano huo uliofanyika mjini Meatu mkoani Simiyu.
Baadhi ya Vijana wa Meatu wakiwa juu ya mti na bendera zao wakipata ujumbe wa Dr John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
Akina mama wakiwa katika mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Dr, John Pombe Magufuli.
Wananchi wakimsikiliza Dr. John Pombe Magufuli wakati alipokuwa akimwaga sera zake.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr.
John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa mkutano mjini Meatu.
Msanii Emmanuel Mbasha akiwa katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment