Watu
takriban milioni moja wamelazimika kuhama makazi yao ChileSerikali ya
Chile imetangaza hali ya dharula katika mji uliokumbwa na tetemeko lenye
nguvu
watu
milioni moja walitakiwa kuacha makazi yao na takriban watu 11 walipoteza
maisha baada ya tetemeko lenye ukubwa wa kipimo cha ritcha 8.3 kupiga
jumatano usiku.
Mji wa pwani,Coquimbo, mawimbi ya futi 15 yalipiga pwani.mawimbi madogo ya Tsunami yalipiga mpaka Alaska.
Rais Michelle Bachelet alitembea Coquimbo alhamisi.
Tetemeko hili ni kubwa zaidi duniani mwaka huu, lilitokea kwa dakika tatu.
Gloria Navarro anayeishi pwani ya mji wa La Serena amesema watu walikuwa wakikimbia hovyo.
Nchini Chile wakazi wameonekana wakifanya usafi siku ya alhamisi baada ya tetemeko linaloelezwa kuwa la sita lenye nguvu.
Kijiji cha Tongoy kiliharibiwa, na zaidi ya nyumba 500 ziliharibiwa vibaya,vikosi vya kupambana na dharula vimeeleza.
Takriban nyumba 90,000 hazina umeme.
No comments:
Post a Comment